Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagombea watatu CCM wapita bila kupingwa

Mon, 24 Sep 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Moshi. Chama cha Mapinduzi (CCM), kimepata ushindi katika kata tatu kati ya tano zilizotangazwa kufanya uchaguzi mdogo wa udiwani katika mkoa wa Kilimanjaro.

Wakati wagombea wa CCM wakipita bila kupingwa katika kata hizo, kada wa SAU, Issack Kireti amejitokeza tena kuwania Udiwani wa Korongoni.

Katibu wa CCM Mkoa Kilimanjaro, Jonathan Mabhia, aliwataja wagombea wao waliopita bila kupingwa kuwa ni John Msofe (Vumari), Shilimiaufoo Simbo (Romu) na Elibariki Mbise wa kata ya Rundugai.

CCM imepita bila kupingwa, baada ya Chadema kujitoa kushiriki chaguzi hizo ndogo.

Hata hivyo, katika kata ya Korongoni Manispaa ya Moshi, mgombea wa CCM, Ally Mwamba atachuana na wagombea kutoka vyama vitatu vya upinzani ambavyo vimesimamisha wagombea.

Wagombea hao ni Vicent Mulamba kutoka NCCR-Mageuzi, Livin Severine (ACT-Wazalendo) na Issack Kireti wa SAU ambaye mwezi uliopita aligombea Kata ya Mawenzi na kushindwa.

Katibu wa Chadema mkoani Kilimanjaro, Basil Lema, alisema kwamba wameamua kutosimamisha wagombea kutokana na tamko la kamati kuu ya Chadema lililoelekeza uamuzi wa chama hicho kujitoa katika chaguzi hizo.

Chanzo: mwananchi.co.tz