Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagombea udiwani wa Chadema mkoani Manyara hawa hapa

11420 Chadema+pic TanzaniaWeb

Sat, 14 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Babati. Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) mkoani Manyara kimewapitisha wagombea watano wa udiwani watakaopeperusha bendera ya chama hicho katika uchaguzi utakaofanyika Agosti 12, 2018.

Akizungumza na MCL Digital leo Jumamosi Julai 14, 2018 katibu wa chama hicho mkoa wa Manyara,  Gervas Sulle amesema wamejipanga ipasavyo kushinda uchaguzi wa kata hizo. 

Amewataja wagombea hao na kata zao katika mabano kuwa ni Mathias Zebedayo (Bagara),  Theophil Lolo (Masakta), Philipo Mallo (Gehandu),  Zacharia Nihhi (Tumati) na Daniel Boa (Hayderer).

Amebainisha kuwa Chadema wamejipanga ipasavyo kushinda katika kata hizo kwa kufanya kampeni za kistaarabu, kusisistiza kuwa endapo uchaguzi utakuwa wa huru na wa haki, wataibuka na ushindi. 

"Kwenye kata nne kati ya tano, Chadema ilikuwa inaongoza udiwani, tunatarajia wananchi wa Manyara watawachagua tena wagombea wetu na kushinda upya uchaguzi huo mapema sana," alisema Sulle. 

Uchaguzi katika kata hizo unafanyika kufuatia madiwani wanne wa Chadema na mmoja wa ACT-Wazalendo kujiuzulu na kuhamia CCM kwa maelezo kuwa wanaunga mkono juhudi za Rais John Magufuli.

Katika mchakato wa kura ya maoni ndani ya CCM, chama hicho tawala kimewapitisha tena wagombea hao waliokuwa madiwani wa Chadema na ACT, kuwania udiwani kwa tiketi ya CCM.

Uchaguzi wa kata 79 na katika jimbo la Buyungu mkoani Kigoma umepangwa kufanyika Agosti 12.

Kwa mujibu wa taarifa ya Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) kampeni  za uchaguzi huo zitaanza kesho Jumapili hadi Agosti 11, 2018.

 

 

 

Chanzo: mwananchi.co.tz