Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagombea ubunge UWT mbaroni rushwa mil 6.7/-

08a5dafc0107b4d7863e6a2eddc48466 Wagombea ubunge UWT mbaroni rushwa mil 6.7/-

Wed, 29 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TAASISI ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (Takukuru), Mkoa wa Rukwa inatarajia kuwashitaki mahamakani wanachama wawili wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa tuhuma za kugawa Sh 6,764,000 kuhonga wajumbe wa Mkutano Mkuu wa Umoja wa Wanawake wa (UWT) na mawakala ili wapigiwe kura.

Watuhumiwa hao, Irene Ndyamkama na Theresia Mzindakaya walikuwa miongoni mwa wanachama wa CCM walioomba kupitishwa kuwa wabunge wa Viti Maalumu.

Aidha watu 13 wakiwemo wajumbe saba wa UWT wa Wilaya ya Kalambo wanatarajiwa kujumuishwa kwenye kesi hiyo.

Akizungumza na waandishi wa habari mjini Sumbawanga jana, Kamanda wa Takukuru, Mkoa wa Rukwa, Hamza Mwenda alisema taasisi hiyo imefanikiwa ‘kuwatemesha’ kiasi cha Sh 6,764,000 ambacho watuhumiwa hao wawili waliwapatia wajumbe ambao wangeshiriki Mkutano Mkuu wa CCM na mawakala.

Alisema Takukuru katika matukio hayo imeokoa kiasi cha Sh 6,764,000/- zilizotolewa kama hongo kwa wajumbe wa UWT- CCM, Wilaya ya Kalambo zikiwemo Sh 604,000/- zilizotolewa na Theresia Mzindakaya. “

Naomba nianze na tukio lililotokea Julai 21 mwaka huu la Takukuru kumkamata mtia nia kwa nafasi ya ubunge wa Viti Maalumu mkoa wa Rukwa, Irene Ndyamkama,”alisema.

Alisema, Julai 20 mwaka huu walipokea taarifa kwa msiri wao kuwa Irene anakusudia kutoa hongo kwa wajumbe wa UWT, Wilaya ya Kalambo ambao wangepiga kura Julai 23 mwaka huu kuchagua wagombea wa nafasi ya ubunge Viti Maalumu, Mkoa wa Rukwa.

Ilidaiwa kuwa fedha hizo zingetolewa nyumbani kwa Yusta Kajema ambaye ni mkazi wa kijiji cha Singiwe wilayani humo.

“Baada ya kupokelewa kwa taarifa hiyo, maofisa wa Takukuru Wilaya ya Kalambo walifika katika kijiji cha Singiwe na kufanikiwa kuwaweka chini ya ulinzi wajume saba wa UWT wakiwa nyumbani kwa Yusta Kajema.

Chanzo: habarileo.co.tz