Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagombea ubunge Chadema hawa hapa

12449 Pic+chademak TanzaniaWeb

Fri, 17 Aug 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) imeteua wagombea wake wa ubunge katika majimbo matatu.

Walioteuliwa na majimbo watakayowania katika mabano ni Asia Msangi (Ukonga), Amina Saguti (Korogwe Vijijini) na Yonas Laiser (Mondulu).

Taarifa ya Chadema iliyotolewa leo Ijumaa Agosti 17, 2018 na mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa chama hicho, Tumaini Makene imesema wagombea hao wamepitishwa katika kikao maalum cha kamati kuu kilichoketi kwa siku mbili kati ya juzi na jana.

“Kamati Kuu ya Chama imefanya uteuzi huo wa wagombea ubunge kwa mamlaka iliyonayo kwa mujibu wa Katiba ya Chama ya mwaka 2006, toleo la mwaka 2016, ibara ya 7.7.16(q),” amesema Makene.

Chanzo: mwananchi.co.tz