Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagombea 4 Viti Maalumu UVCCM watupwa nje

2cb66340e58f1d58017372b40615219f Wagombea 4 Viti Maalumu UVCCM watupwa nje

Sat, 8 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KAMATI ya Utelekezaji ya Baraza Kuu la Umoja wa Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UV-CCM) Taifa, imebaini wagombea wanne wa Ubunge Viti Maalumu wamevunja kanuni ya jumuiya hiyo.

Kutokana na kuvunja kanuni, jumuiya hiyo imechukua uamuzi wa kuwachukua washindi wa pili wa kura za maoni kwenye mikoa husika ambao wamekidhi vigezo.

Uamuzi wa jumuiya umesemwa na Kaimu Mkuu wa Idara ya Uhamasishaji na Chipukizi UV-CCM Taifa, Leonard Singo jijini hapa jana.

Singo alikuwa akizungumzia maandalizi ya Mkutano Maalumu wa Baraza la UV-CCM Taifa ambao unafanyika leo jijini hapa kwa ajili ya kuchagua viongozi hao kupitia kundi la vijana.

Hata hivyo Singo, hakutaka kuweka wazi majina ya wagombea hao na kudai kuwa kwa sasa ni siri ya vikao.

Alisema mchakato huo umekwenda vizuri kwa kuzingatia kanuni na miongozo ya Jumuiya hiyo.

Chanzo: habarileo.co.tz