Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wagombea 33 wa CCM wajitosa kumrithi Joshua Nassari

Wed, 3 Apr 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Arusha. Wanachama 33 wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) wamechukua na kurejesha fomu za kuomba wapitishwe kugombea ubunge wa Arumeru Mashariki mkoa wa Arusha katika uchaguzi mdogo utakaofanyika Mei 19, 2019.

Katibu mpya wa CCM wilaya ya Meru, Shaban Mdoe ambaye pia ni Katibu Mwenezi wa mkoa wa Arusha akizungumza na Mwananchi alisema hadi jana saa 10 jioni mchakato wa kuchukua na kurejesha ulipofungwa wanachama hao 33  wamejitosa kuwania kupitishwa kuwania nafasi hiyo.

Ni majina matatu ambayo yalikua yamefahamika ambayo ni Rehema  Mrosso,Julius Mungure aliyewahi kuwa mjumbe wa halmashauri Kuu, na Dk. John Pallangyo ambaye ni Mwenyekiti wa Wazazi mkoa wa Arusha.

Mdoe alisema kesho Alhamisi Aprili 4, 2019 utafanyika mkutano wa chama hicho wilaya na kamati ya siasa ya wilaya itakutana  Aprili 8, 2019.

Uchaguzi huo unafanyika baada ya aliyekuwa mbunge wa jimbo hilo kupitia Chadema, Joshua Nassari kupoteza sifa za kuwa mbunge kutokana na kutokuhudhuria vikao vya mikutano mitatu ya Bunge bila ya kutoa taarifa.

Mikutano hiyo ni ule wa 12 wa Septemba 4 hadi 14 mwaka 2018, mkutano wa 13 wa Novemba 6 hadi 16 mwaka 2018 na mkutano wa 14 wa 29 Januari hadi Februari 9 mwaka 2019.



Chanzo: mwananchi.co.tz