Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wafuasi wa Chadema wadhibitiwa, washindwa kingia mahakamani

Wafuasi Wafuasi wa Chadema

Fri, 6 Aug 2021 Chanzo: Mwananchi

Jeshi la Polisi limeimarisha ulinzi nje ya Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu na kwenye barabara zilizopo jirani kuhakikisha wafuasi wa Chadema hawakusanyiki wakati kesi ya mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe ikiendelea.

Mbowe anayekabiliwa na kesi ya uhujumu uchumi amefikishwa mahakamani hapo leo Ijumaa Agosti 6, 2021 akiwa na washtakiwa wengine watatu.

Mapema asubuhi askari waliovalia sare na nguo za kawaida walisambaa kwenye njia zote za kuingilia mahakamani huku nje ya geti yakiwa yameegeshwa magari ya maji ya kuwasha na mengine yenye askari.

Hata hivyo Mwananchi imeshuhudia askari wakihoji wanachama waliovalia sare za Chadema na kuwaamuru kurudi walikotoka huku magari yenye watu waaliovaa sare yakizungukazunguka nje ya mahakama.

Katika geti la kuingilia ndani askari waliovalia sare na nguo za kawaida wameonekana wakihojiwa na kutakiwa kuonyesha vitambulisho ambapo watu wachache ndio waliofanikiwa kuingia ndani.

Miongoni mwa waliohudhuria ni pamoja na katibu mkuu John Mnyika, Mwenyekiti wa NCCR Mageuzi, James Mbatia, Kiongozi wa ACT Wazalendo, Zitto Kabwe na aliyekuwa mbunge wa Mbeya Mjini, Joseph Mbilinyi.

Chanzo: Mwananchi