Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wadau: Mwaka 2022 umeacha pengo la kisiasa

CHADEMAAA UHUNIU KANUNIII Wadau: Mwaka 2022 umeacha pengo la kisiasa

Thu, 29 Dec 2022 Chanzo: Mwananchi

Mdau wa masuala ya siasa na jamii, Gwangway Ole Yo amesema mwaka 2022 uliopo ukingoni umeacha pengo katika siasa hasa mikutano ya hadhara ambayo bado haijaruhusiwa.

Hata hivyo, Ole Yo amesema mwaka 2022 ulikuwa na mwanga hasa katika maridhiano kati ya chama cha tawala na vyama vya upinzani ikiwemo chama kikuu cha upinzani cha Chadema.

Kwa nyakati tofauti mwaka huu, Rais Samia Suluhu Hassan ambaye pia ni mwenyekiti wa CCM amekuwwa akikutana na kufanya mazungumzo na viongozi wa vya upinzani ikiwemo ni sehemu ya kuimarisha demokrasia nchini.

Ole Yo amesema hayo janaJumatano, Desemba 28, 2022 katika mjadala wa ‘Twitter Space’ ulioandaliwa na Mwananchi Communication Limited (MCL), uliokuwa na mada ya mwaka 2022 ulikuwaje kwa Watanzania katika kiuchumi, siasa na jamii?

“Tunafunga mwaka 2022 kukiwa bado kuna pengo la mikutano ya hadhara, bado kuna changamoto, ingawa kumekuwa na hatua kubwa ya maridhiano kati ya CCM na vyama vya upinzani. Lakini bado hatujui matokeo yake itakuaje, ingawa ni jitihada nzuri,”amesema Ole Yo.

Mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa ilipigwa marufuku tangu mwaka 2016, katika Serikali ya awamu tano na imekuwa ikifanyika wakati wa kampeni za uchaguzi mkuu au chaguzi za marudio.

Hata hivyo, kwa nyakati tofauti Chadema, kimekuwa kikishinikiza kwa Serikali kuruhusu au kuondoa zuio hilo, wakisema lipo nje ya Kikatiba.

Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM), Dk Aviti Mushi alimuomba Rais Samia kuruhusu mikutano ya hadhara ili kusikiliza mawazo mbadala hasa kwa kuwapa maagizo polisi kuondoa zuio hilo.

Chanzo: Mwananchi