Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge waliohama CUF kukampeni CCM

A79c48088005193b98661198f668922f Wabunge waliohama CUF kukampeni CCM

Mon, 20 Jul 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

WABUNGE waliohama Chama Cha Wananchi (CUF) na kujiunga na Chama Cha Mapinduzi (CCM) wameahidi kumuunga mkono mgombea wa CCM katika uchaguzi wa Rais Zanzibar, Dk Hussein Mwinyi kwa kuwa ni mwadilifu na mchapa kazi anayeweka mbele maslahi ya taifa.

Mohamed Juma Ngwali aliyekuwa Mbunge wa Wawi kupitia CUF aliwaambia wananchi jana kuwa amekuwa na mgombea Dk Mwinyi kwenye Bunge la Tanzania vipindi viwili hivyo anamfahamu ni mchapakazi, mbunifu mwenye uwezo wa kufanya uamuzi akiongoza Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa miaka 10.

‘’Wananchi wa Kisiwa cha Pemba tusifanye makosa... tumchagueni mgombea wa CCM na kukipa ushindi ili kilete maendeleo,’’alisema.

Aliyekuwa Mbunge wa CUF Chake Chake, Kaizer Yussuf Makame aliwataka wananchi wa Pemba kutowachagua wapinzani ambao hawana jambo la maendeleo wanalowafanyia wananchi.

Alisema muda mrefu wapinzani wanachaguliwa lakini wakishika nafasi hizo hakuna anayekuja katika jimbo lake kwa ajili ya kusimamia maendeleo na wanabaki Dar-es-Salaam tu.

‘’Wananchi wa Pemba wamekuwa nyuma kimaendeleo katika majimbo ya uchaguzi kwa sababu wamekuwa wakiwachagua wapinzani ambao hawashirikiani na serikali iliyopo madarakani ili kuleta maendeleo, ‘’alisema.

Juma Hamad aliyewahi kuwa Waziri wa Maliasili serikali ya awamu ya pili alisema huu ni mwaka kwa wananchi wa Pemba kufanya uamuzi sahihi kuichagua CCM kuongoza dola kwa kushika majimbo yote Kisiwani Pemba.

Alisema Dk Hussein ana uwezo wa kutosha kuongoza Zanzibar na kuleta mabadiliko ya uongozi kwa kuwaunganisha wananchi wote. ‘’Wananchi kisiwani Pemba tusifanye makosa ..... tumchague Dk Hussein na wawakilishi na wabunge wa CCM kuleta maendeleo ya wananchi Unguja na Pemba na kuvunja ukanda wa Waunguja na Wapemba, ‘’alisema.

Awali Naibu Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar, Dk Abdalla Juma Sadalla Mabodi alisema wabunge wastaafu waliojiunga na CCM kutoka CUF watatumika kikamilifu kuhamasisha wananchi kuiunga mkono CCM ishinde huko.

Chanzo: habarileo.co.tz