Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge wa CCM walalamikia Serikali kuchukua vyanzo vya halmashauri

63339 Pic+wabunge

Wed, 19 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Kigoma Kusini (CCM), Husna Mwilima amesema hali ya halmashauri ni mbaya baada ya Serikali kuu kuchukua vyanzo vyao vingi.

Akichangia mapendekezo ya Bajeti ya Serikali kwa mwaka wa fedha 2019/2020, jana Jumanne Juni 18 2019, Husna amesema alifikiri katika Sheria ya Fedha (Finance bill) ya mwaka huu wangerejesha kodi hiyo ya majengo kwa halmashauri.

Amesema Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka wa Mapato Tanzania (TRA) aliwaambia wameweza kukusanya kodi hiyo katika halmashauri 30 kati ya 180.

“Kwanini tusirudishe kwa halmashauri, halmashauri zetu hali ni mbaya,” amesema.

Kauli hiyo iliungwa mkono na Mbunge wa Lulindi (CCM), Jerome Bwanausi ambaye alisema walivyokuwa wakikusanya halmashauri walikuwa wakifanya vizuri.

“Tulikuwa tunafanya vizuri baada ya kushuka, TRA ninaona kushuka kwa kiwango cha ukusanyaji wa property tax (kodi ya majengo,” amesema.

Pia Soma

Amesema Watanzania wako tayari kulipa lakini mamlaka ambazo zimepewa wajibu huo hazitilii umakini ukusanyaji huo.

Amesema kama wakitilia umakini suala hilo ni eneo ambayo watapata kodi nyingi.

Chanzo: mwananchi.co.tz