Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge wa CCM kuchagua wagombea wa EALA

Wabungeepiic Data Wabunge wa CCM kuchagua wagombea wa EALA

Sat, 10 Sep 2022 Chanzo: www.mwananchi.co.tz

Wabunge wa CCM leo Jumamosi, Septemba 10, 2022 watafanya uchaguzi wa ndani wa wagombea wa ubunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), kabla ya kwenda kupigiwa kura na wabunge wote Septemba 13,2022.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa Itikadi na Uenezi jana, Shaka Hamidu Shaka wagombea wote waliopendekezwa na Kamati Kuu ya CCM wanatakiwa kuwepo Dodoma.

Amesema kikao kilichowateua na kuwapendekeza kilifanyika jijini Dar es Salaam, chini ya Mwenyekiti wa CCM, Rais Samia Suluhu Hassan, Septemba 7, 2022.

“Kwa mujibu wa kanuni za CCM za uteuzi wa wagombea wa CCM katika vyombo vya dola, uteuzi wa wagombea nafasi za ubunge wa Afrika Mashariki utafanywa na kamati ya wabunge wote wa CCM,” amesema Shaka.

Shaka amesema jumla ya wanachama 16 wameteuliwa na kupendekezwa kuwania nafasi tano za ubunge wa EALA ambapo kati ya nafasi hizo watatu ni wanaume na wawili wanawake.

Amewataja wanaume walioteuliwa na kupendekezwa na Kamati Kuu pamoja na Dk Gilbert Bankobeza, Anar Kachwamba, Benedict Kivove, Dk Ng’waru Maghembe, Gidion Mandesi na Methusela Mbajo.

Wengine ni Brigedia Jenerali Marianus Mhagama, Balozi James Msekela, Dk Leonard Subi na James Millya.

Kwa upande wa wanawake, walioteuliwa na CC kuwania nafasi mbili ni Theddy Patrick, Angela Kizigha, Dk Shogo Mlozi, Doris Mollel, Amina Mgeni na Jalia Mayanja.

Shaka amesema kwa upande wa Zanzibar, wabunge hao wa CCM watateua na kupendekeza wanachama watatu ambapo wawili watakuwa wanaume na mmoja mwanamke.

Amewataja wanaume walioteuliwa kuwania nafasi hizo tatu ni Machano Ali Machono, Abdulla Hasnuu Makame, Mmanga Miengo Mjawiri, Mourice Oscar Bendera, Haji Vuai Ussi, Faki Ame Kesi.

Kwa upande wa wanawake kutoka Zanzibar, Shaka amewataja waliopitishwa na CC, kuwa ni Lulua Salum Ali, Nadra Juma Mohamed, Maryam Said Mussa na Rahma Mohamed Ibrahim.

Chanzo: www.mwananchi.co.tz