Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge Tanzania wataka wabakaji wahasiwe, AG awatetea

94354 Wabakaji+pic Wabunge Tanzania wataka wabakaji wahasiwe, AG awatetea

Tue, 4 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Swali la kutaka wanaume wanaobaka watoto waasiwe limeibua mjadala mkali bungeni huku Mwanasheria Mkuu wa Serikali ya Tanzania (AG), Profesa Adelardus Kilangi akaingilia kati akisema hawawezi kuwahasi.

Hayo yamejiri leo Jumanne Februari 4, 2020 bungeni ambapo Mbunge wa Viti maalumu (CCM) Zainabu Katimba ameibua swali hilo ambalo lilipigiwa makofi na wabunge na kuwafanya mawaziri kusimama pamoja na Profesa Kilangi.

Katambi ameitaka Serikali ya Tanzania itamke ni kwa nini isiwahukumu kwa kuhasiwa wanaume ambao wanaendelea na vitendo vya ubakaji kwa kuwa adhabu zilizopo hazitoshi.

Akijibu swali hilo, Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Agustine Mahiga amesema adhabu iliyopo kwa sasa ya miaka 30 inatosha lakini akapendekeza kama mbunge anaona ni ndogo alishauri Bunge kutunga sheria.

Naye Profesa Kilangi amesema kuwahasi watu ni kukiuka Katiba ya nchi ibara ya 13 (6) ambayo inazuia mtu kuteswa na kudhalilishwa utu wake hivyo kuweka adhabu hiyo itakuwa ni kinyume na Katiba.

Baada ya majibu hayo, Mwenyekiti wa Bunge, Najma Giga alimtaka Profesa Kilangi kutafakari upya kwani wabakaji nao wanavunja katiba hiyo hivyo haiwezekani kulinda upande mmoja.

Pia Soma

Advertisement

Kwa upande wake, Waziri wa afya, Ummy Mwalimu amesema jukumu la kulinda watoto ni la wazazi wenyewe hivyo na kuomba Watanzania wasikwepe jukumu hilo.

Waziri Ummy amesema wazazi na walezi wanapaswa kuwa karibu na watoto wale na kujenga urafiki ili kuhakikisha kile ambacho wanafanyiwa waweze kuwaeleza pasina kuwaogopa.

Chanzo: mwananchi.co.tz