Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge Tanzania waanza kuipigia kura bajeti ya serikali

10108 Kura+pic TZW

Wed, 27 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Shughuli ya upigaji kura kwa Bajeti ya Serikali ya mwaka 2018/19 ya Sh32.45 trilioni inaendelea bungeni jijini Dodoma.

Mara baada ya kuingia ukumbini leo jioni Juni 26 Spika wa Bunge Job Ndugai amesema, “leo ni full house.” Akimaanisha ukumbi umejaa.

 “Kwa kweli mahudhurio ya leo ni mazuri kwani hata mheshimiwa Mbunge wa Momba-Chadema, David Silinde amerudi kwani alikuwa haonekani.”amesema na kuongeza:

“Wale wanaotembea tembea, watulie ili zoezi letu liweze kuendelea vizuri.”

Amesema jumla ya wabunge wote ni 392  na Katibu wa Bunge, Stephen Kagaigai amesema jumla ya wabunge waliopo ndani ni 303 na ili upigaji kura ufanyike wanahitajika kuwa nusu yao.

 

“ Utaratibu wa upigaji kura utaanza kwa kuitwa viongozi waliopo humu ndani, mawaziri, wenyeviti wa kamati za Bunge na wabunge wengine,” amesema Kagaigai

 

Miongoni mwa mawaziri ambao hawapo leo ni; Dk Agustine Mahiga (Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Kikanda na Kimataifa) na Profesa Palamagamba Kabudi wa Katiba na Sheria pamoja na Kiongozi wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, Freeman Mbowe.

Chanzo: mwananchi.co.tz