Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge Kagera wapinga Mkoa wao kumegwa na kupelekwa Chato

Wapinzani Pic Data.jpeg Wabunge Kagera wapinga Mkoa wao kumegwa na kupelekwa Chato

Thu, 4 Nov 2021 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Wabunge wa Mkoa wa Kagera, Wamepinga kitendo cha kuendelea kuumega Mkoa wa Kagera. Hii imekuja baada ya Kuanzishwa Mchakato wa kufanya Wilaya ya Chato iliyopo Geita kuwa Mkoa.

Mkuu wa Mkoa wa Geita, Rosemary Senyamule, alisema Kamati ya Ushauri ya Mkoa wa Geita (RCC) ilipendekeza wilaya tano, Chato na Bukombe mkoani Geita. Biharamulo na Ngara mkoani Kagera na sehemu ya Wilaya ya Kakonko mkoani Kigoma zichukuliwe kwa ajili ya kuanzisha Mkoa mpya wa Chato.

Kwa mujibu wa takwimu za sensa ya mwaka 2012, idadi ya wakazi wa Wilaya ya Chato ilihesabiwa kuwa 365,127. Chato ilianzishwa mwaka 2007 kutokana na maeneo ya Wilaya ya Biharamulo, Mkoa wa Kagera, mwaka 2012 ikasogezwa katika mkoa mpya wa Geita.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live