Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge Chadema walazwa Aga Khan, polisi wakanusha kuwapiga

99034 Pic+wabunge Wabunge Chadema walazwa Aga Khan, polisi wakanusha kuwapiga

Mon, 16 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Wakati Chadema wakisema wabunge wake watatu wamelazwa hospitali  ya Aga Khan baada ya kupigwa na polisi, Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilala, Zuberi Chembela amesema hakuna mwanachama wa chama hicho kikuu cha upinzani nchini Tanzania waliyempiga kwa kuwa hilo si jukumu lao.

“Jukumu la polisi sio kupiga watu. Hao wanachama wa Chadema hawajapigwa na polisi labda waseme kuna waliowapiga lakini sio polisi, “ amesema Chembela alipoulizwa na Mwananchi kuhusu madai hayo ya Chadema.

Akizungumza na Mwananchi leo Jumamosi Machi 14, 2020 Mkurugenzi wa Itikadi, Uenezi, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa Chadema, John Mrema amewataja wabunge hao kuwa ni

 Ester Bulaya (Bunda), Halima Mdee (Kawe) na Jesca Kishoa (Viti Maalum).

Amesema ni miongoni mwa watu takribani 27 waliokamatwa jana Ijumaa Machi 13, 2020 walipofika katika gereza la Segerea kumchukua mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe aliyekuwa akitoka jela baada ya kukamilisha utaratibu wa kulipa faini ya Sh70 milioni.

Amesema viongozi hao walipelekwa  kituo cha polisi Stakishari walikotoa maelezo na kuachiwa kwa dhamana, “walipelekwa Hospitali ya Aga Khan kwa matibabu kwa kuwa walikuwa na majeraha sana, wameumizwa. Tumetuma viongozi wetu wanafuatilia kwa sasa bado asubuhi baada yakupata taarifa ya hali zao tutawafahamisha.”

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
Mrema amesema Mdee na Bulaya wamelazwa Aga Khan na Kishoa amelazwa Hospitali ya Amana.

Hata hivyo, mkuu wa idara ya masoko na mawasiliano wa hospitali ya Aga Khan,  Olayce Steven amesema,” waliopo hospitali ni Halima Mdee na Jesca Kishoa. Wapo chini ya uangalizi wa madaktari na wauguzi na hali zao zinaendelea vizuri. Sina taarifa za Bulaya kulazwa katika hospitali yetu labda kiulizwe chama.”

Chanzo: mwananchi.co.tz