Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge CCM wamuaga Kinana

9581 Kinana+pic TZWeb

Wed, 20 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mwenyekiti wa Kamati ya Wabunge wa CCM, Kassim Majaliwa amemkaribisha Katibu Mkuu wa chama hicho, Dk Bashiru Ally na kumuaga mtangulizi wake Abdulrahman Kinana.

Majaliwa ambaye pia ni Waziri Mkuu amesema ushirikiano uliopo baina ya wabunge wa chama hicho ni nguzo ya ushindi katika uchaguzi.

Amemhakikishia uchaguzi wa serikali za mitaa utakaofanyika mwakani wataibuka kidedea.

Waziri Mkuu Majaliwa amesema hayo Juni 19, 2018 katika hafla iliyoandaliwa na wabunge wa CCM jijini Dodoma.

Majaliwa amesema ushirikiano uliopo baina ya wabunge umefanikisha ushindi wa CCM katika uchaguzi mkuu mwaka 2015 chini ya Kinana, huku akimuahidi Dk Bashiru kuendeleza ushirikiano huo.

“Ili tushinde jitihada za mbunge ni kubwa na hatuko tayari kupoteza kiti chochote katika maeneno yoyote yale,” amesema Majaliwa.

Amesema, “Tutakulinda, tutakusemea na wabunge wako tayari kukupigania. Tutashinda uchaguzi wa serikali za mitaa. Tukuhakikishie uko katika mikono salama.”

Majaliwa amesema wanamshukuru Kinana kwa kuwa wamefanya naye kazi kwa weledi, jitihada na kwa mafanikio makubwa.

Akizungumza kwa niaba ya Kamati ya wabunge wa CCM, Margaret Sitta amesema kama wangeulizwa bungeni, wanaosema Kinana astafuu hajui ambaye angesema ndiyo ila wengi wangesema siyo, huku akiungwa mkono na wabunge waliosema "siyooooooo"

“Ulitupenda, ulitutetea na ulikuja kwetu na kutusikiliza. Kinana ulikipenda chama na kama mtakumbuka alipokuwa katibu mkuu alikitumikia chama kwa moyo wote na alipopata ukatibu mkuu alizunguka nchi nzima, alichangamsha chama ndiyo ukweli wenyewe,” amesema Sitta.

Amesema, “Ulikuwa mkweli, ulisaidia kukosoa, ulitusifia na kuhimiza sana kutumikia wananchi… asante sana baba ulichangamsha na ulihiimiza tuimarishe chama na kuwa wamoja na kushikamana.”

 

Chanzo: mwananchi.co.tz