Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge CCM kunyoosha njia ya Uspika wa Dk.Tulia

Tuliapicc Data Dk. Tulia Ackson Naibu Spika Tanzania

Mon, 31 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Kamati ya wabunge wa CCM leo itakaa jijini Dodoma kucha-gua jina la mgombea uspika huku Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM ikiwa imepitisha jina moja la Dk Tulia Ackson.

Dk Tulia ambaye pia ni Naibu Spi-ka wa Bunge na Mbunge wa Mbeya Mjini, alipitishwa kuwania nafasi hiyo na Kamati Kuu ya Halmashauri Kuu ya CCM Januari 20,2022,hivyo kuwa mgombea pekee wa chama hicho kuwania kiti cha Spika kili-choachwa wazi na Job Ndugai ali-yejiuluzu Januari 6,2022.

"Naomba kutoa taarifa kwa uma wa Watanzania kuwa nimeandika barua kwenda kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) kujiuzulu nafasi ya Spika wa Bunge la Jamhuri wa wa Tanzania kwa hiari,” ilieleza taarifa Ndugai kwa umma.

Ndugai alijiuzulu siku chache baada ya kutoa kauli iliyozua mta-faruku kuhusu mikopo inayochuku-liwa na Serikali.

Dk Tulia alikuwa akishindana na wagombea wengine 69 ndani ya CCM wlioomba kupitishwa na chama chao kuwania nafasi ya kiti hicho.

Uratibu wa CCM ni kupeleka majina yasiyozidi matatu kwenye kamati ya wabunge,lakini Kamati Kuu iliamua kwenda na jina moja la Dk Tulia.

Hivyo ni wazi kuwa Dk Tulia sasa anakuwa mwanamke wa pili kuwa Spika kama atachaguliwa na wabunge hao kwenda kuwania kiti hicho ndani ya Bunge na akashinda.

Katibu wa Wabunge wa CCM, Rashid Shangazi alisema uchaguzi huo utafanyika leo saa 8:00 mchana.

Alipoulizwa inapotokea CCM imeleta jina moja la mgombea inakuwje,Shangazi alisema ucha-guzi huo unaongozwa na kanuni, hivyo wataangalia kanuni zao zinasemaje.

"Tunafanya kesho(leo) mchana saa 8..Tutaangalia kanuni kesho (leo) zinasemaje kuhusu jambo hilo,"alisema Shangazi.

Hadi sasa chama cha upinzani ambacho kimejitokeza kuwania kiti hicho ni cha Alliance for Democratic Change (ADC) ambacho kimempi-tisha Maimuna Kassim kuwania nafasi hiyo ndani ya Bunge.

Miongoni mwa wana-CCM wali-oshindana na Dk Tulia ambao ni wabunge ni Mussa Azzan Zungu (Ilala),Luhaga Mpina (Kisesa), Stella Manyanya (Nyasa), God-win Kunambi (Mlimba) na Joseph Musukuma (Geita Vijijini).

Pia, walikuwamo wabunge wa zamani,Stephen Masele (Shinyan-ga Mjini),Athuman Mfutakamba (Igalula), Andrew Chenge (Bariadi Magharibi), Profesa Norman Sigalla (Makete), Dk Titus Kamani (Buse-ga), Ezekiel Maige (Masalala) na Sophia Simba(Viti Maalum).

Kwnye kinyang'anyiro hicho pia kulikuwa na Katibu wa Bunge wa zamani, Thomas Kashilillah na watumishi wa umma, makada, viongozi wa zamani wa Serikali na wanafunzi wawili wa vyuo vikuu.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live