Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge: Asante JPM kumtua mama ndoo

339eac1584e0864aa40d68a9167dd3cc Wabunge: Asante JPM kumtua mama ndoo

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: habarileo.co.tz

WABUNGE wamesema Rais John Magufuli ameandika historia kwa kutenga fedha, kuanzisha miradi mingi ya maji iliyofanikisha azma ya kumtua mwanamke ndoo kichwani.

Waliyasema hayo jana bungeni jijini Dodoma wakati wakichangia hoja iliyowasilishwa na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa, kujadili hotuba ya Rais Magufuli aliyoiwasilisha wakati akizindua Bunge la 12 Novemba 13, mwaka jana.

Mbunge wa Viti Maalumu, Juliana Shonza (CCM), alisema Rais Magufuli ameandika historia kwa kuweka fedha nyingi zaidi ya Sh trilioni 2.2 katika miradi ya maji ili kutatua changamoto ya maji kwa wananchi hasa wanawake na watoto waliokuwa wakitembea umbali mrefu kutafuta huduma hiyo.

Shonza alisema katika miaka mitano iliyopita serikali ilijenga miradi 1422 ya maji iliyosaidia kupunguza kero ya maji. Mbunge huyo aliyoushauri kwa serikali kwamba kama imedhamiria kumaliza kero ya maji basi iongeze fedha kwenye Mfuko wa Maji ambao ndicho chanzo pekee cha fedha za kutekeleza miradi.

Mbunge wa Viti Maalumu, Anatropia Theonist (Chadema) alitaka kujua ni kwa kiwango gani serikali imetatua changamoto za maji tangu imeahidi mwaka 2015 ilipoahidi atafanya kampeni ya kumtua ndoo kichwani mwanamke.

Mbunge wa Viti Maalumu, Agnes Mathew (CCM), alisema kampeni ya kumtua mwanamke kichwani imepunguza muda wa kusubiri kupatikana maji baada ya huduma hiyo kusogezwa kwa wananchi.

Mbunge wa Viti Maalumu, Zaituni Swai (CCM) alimpongeza Rais Magufuli kwa kutekeleza miradi mikubwa ya maji ukiwemo wa Arusha wenye thamani ya Sh bilioni 520.

Aliomba serikali itafute vyanzo vingine vya vya maji vikiwemo visima ili kuwapatia maji wananchi wa maeneo mengine kama ya Kata ya Ndurume Arumeru.

Chanzo: habarileo.co.tz