Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Wabunge 19 waliovuliwa uanachama CHADEMA waingia Bungeni

Screenshot 2021 02 02 At 12.46.58 660x400.png Wabunge 19 waliovuliwa uanachama CHADEMA waingia Bungeni

Thu, 4 Feb 2021 Chanzo: millardayo.com

Wabunge 19 wa Viti Maalumu kutoka Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), asubuhi hii wamefika na kuendelea na kikao cha Bunge kilichoanza leo Jumanne, Februari 2, 2021 Jijini Dodoma.

Wabunge hao wakiongozwa na Halima Mdee wameingia mjengoni wakiwa wamevalia mavazi meusi huku Mdee akiwa amevaa barakoa kwa lengo la kujikinga na maambukizo ya virusi vya corona.

Itakumbukwa Wabunge hao tayari walishavuliwa uanachama na chama chao mwishoni mwa mwaka jana kwa madai ya kukiuka utaratibu wa chama chao.

LIVE : RAIS MAGUFULI “WANANCHI WANALIA KWA HUKUMU AMBAZO HAWAWEZI KUZISOMA, MUWAONEE HURUMA”

Chanzo: millardayo.com