Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Waandishi wa habari wazuiwa uchaguzi CCM Kagera

CCM WEB Waandishi wa habari wazuiwa uchaguzi CCM Kagera

Tue, 22 Nov 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Baadhi ya waandishi wa habari wamezuiliwa kuingia kwenye ukumbi wa uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Mkoa wa Kagera huku ikielezwa kuna waandishi wamealikwa kwa ajili ya kuandika habari katika uchaguzi huo.

Mmoja wa watu waliokuwa mlangoni akiruhusu wajumbe kuingia ukumbini katika uchaguzi huo unaofanyika leo Jumanne, Novemba 22, 2022 amekuja na majina ya vyombo vitano akisema waandishi wake wanaruhusiwa kuingia ukumbini huku wengine wakizuiliwakuingia.

Katibu wa CCM mkoa wa Kagera, Christopher Palangyo alipofuatwa na waandishi hao alidai wasubiri watapata utaratibu badaye na hadi wagombea wanajinadi waandishi hao walikuwa nje ya ukumbi.

Wagombea nafasi ya uenyekiti CCM Mkoa wa Kagera ni Novatus Nkwama, Medard Mshobozi, Nazir Kalamagi na Kostansia Buhiye na msimamizi wa uchaguzi huo ni Spika wa Bunge la Tanzania, Dk Tulia Akson.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live