Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

WATIA NIA CCM WATAKIWA KUWA NA MASHIRIKIANO

Image 323.png?fit=783%2C570 WATIA NIA CCM WATAKIWA KUWA NA MASHIRIKIANO

Wed, 19 Aug 2020 Chanzo: zanzibar24.co.tz

Mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa Sufiani Ramadhani Khamis amewataka waliotia nia ya kuomba kuteuliwa nafasi za ubunge, uwakilishi, viti maalum na udiwani kupitia tiketii ya Chama cha Mapinduzi kuwa na mshikamano mara baada ya kutangazwa majina ya wateule.

Kauli hiyo ameitoa kikao cha pamoja alipokutana wa watia nao hao zaidi ya mia 400 waliojitokeza kuomba nafasi hizo katika wadi, majimbo ndani ya  Mkoa wa Mjini (kichama) katika ukumbi wa ccm Mkoa wa Mjini.

Sufiani amesema watia nia wote wameonyesha mapenzi makubwa katika kukitumikia chama hivyo umoja na ushirikiano lazima kudumishwa ili kuhakikisha chama cha mapinduzi kinapata ushindi katika uchaguzi mkuu wa tarehe 28 mwezi wa kumi mwaka huu.

Nae Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Mjini Kichama Talib Ali Talib amesema yatapotangazwa majina  baada ya mchujo kwa mujibu wa katiba na kanuni za chama kwa wale ambao majina yao hayatarudi watatakiwa kuwaunga mkono wagombea kwa lengo la kujenga misingi imara ya chama cha mapinduzi.

Aidha amesema kwa wale waliokuwa majina yao hayakurudi watakuwa ndio timu ya kampeni katika jimbo husika kwa katika kufanikisha mchakato wa uchaguzi kuelekea kukipatia chama ushindi  wa ushindi kwa ngazi za udiwani, uwakilishi, ubunge na nafasi ya rais wa zaznibar na ile ya jamhuri ya muungano wa tanzania

Chanzo: zanzibar24.co.tz