Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vyuo vikuu waeleza kwa nini Magufuli achaguliwe tena

1764910d4a8bd08846888f4c0541bfcd Vyuo vikuu waeleza kwa nini Magufuli achaguliwe tena

Mon, 28 Sep 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) seneti ya vyuo na vyuo vikuu mkoani Mbeya, imesema Watanzania wana kila sababu ya kumchagua kwa mara nyingine John Magufuli aendelee kuwa Rais wa Tanzania kwa miaka mingine mitano kutokana na utendaji kazi wake ulioiwezesha nchi kupata heshima ya kipekee.

Wajumbe wa seneti hiyo walibainisha hayo walipochangia mada ya ‘Kwa nini Magufuli tena’ katika Ukumbi wa Mkapa jijini Mbeya. Mwenyekiti wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Chuo Kikuu cha Mzumbe Tawi la Mbeya, Ferdinand Kitole alisema jamii inapozungumza kuhusu kiongozi anayefaa ni lazima imuangalie mtu aliye na ujasiri, uwazi na hofu ya Mungu sifa ni kwamba Magufuli ana sifa hizo.

“Kiongozi lazima ajenge kuaminika ndani ya jamii anayoiongoza...na hili amefanya kwa kujiepusha na wala rushwa ambao wangemsababishia miradi mingi ya kimaendeleo kukwama. Lakini pia kutozurula nje ya nchi kumemuongezea sifa kwa wananchi kuona huyu ni mtu anaelia na na sisi kucheka nasi,”alisema Kitole.

Mwenyekiti wa UVCCM Chuo Cha Afya Cha K’s, Benita Simon alisema uamuzi wa serikali kuboresha sekta ya afya kwa kujenga miundombinu na kununua mashine za matibabu, kumewapunguzia Watanzania mzigo wa kusafiri kwenda mataifa yaliyoendelea kufuata tiba.

Mchangiaji mwingine, Frank Adriano alisema Magufuli amekuwa Rais mzalendo kwa kuwajali na kuwaamini wataalamu Watanzania hata akafikia kuwapa zabuni za kutekeleza miradi ukiwemo ujenzi wa miundombinu zikiwemo barabara.

“Miradi mingi awamu hii tumeshuhudia inajengwa na Watanzania.Tumeona hata Ikulu ya Chamwino pale Dodoma inajengwa na Watanzania wenyewe. Lakini pia ni vigumu kumpa mtu mmoja mmoja fedha lakini kupitia vikundi watu wamekopeshwa fedha na serikali,” alisema Adriano.

Godfrey Joseph aliipongeza serikali kwa kuondoa safari zisizo za lazima kwenda nje, akisema hatua hiyo imesababisha fedha nyingi kuelekezwa kwenye miradi ya maendeleo, ambayo kimsingi ina tija kubwa, tofauti na safari zilizokuwa zikiwaneemesha watu wachache.

Agustino Mpelembwa kutoka Chuo Kikuu Cha Mtakatifu Agustino, Mbeya, alisema hauwezi kuficha moto kwenye nyasi kavu zikabaki salama kwa kazi alizofanya Magufuli watanzania wanapaswa kuonesha mataifa jirani kuwa wana Rais sahihi.

Waziri Mkuu wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Kikuu Cha SAUT, Michael Luoga alisema ni Magufuli aliyerejesha heshima ndani ya CCM, hata wanachama wake leo hii wanapovaa nguo za chama wanajivuna, tofauti na mwaka 2015 ambapo walipata shida kuzivaa mitaani.

Alisema, kama mataifa mengine yanatamani Magufuli akawe Rais wao kwa nini Watanzania wasiendelee kumpa kazi ya kuwatumikia kwa miaka mingine mitano ili miradi kama ya SGR, ya umeme na barabara izidi kumiminika. Rais mstaafu wa Serikali ya Wanafunzi Chuo Cha Afya, Rufaa Mbeya, Kapuya Said alisema hatua ya kuokoa fedha kwa kuwaondoa wafanyakazi hewa waliokuwa wakilipwa mabilioni ya fedha, kiliipa heshima kubwa Serikali ya Magufuli.

Chanzo: habarileo.co.tz