Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vyama vyakabidhiwa wapigakura

19c4732f7091dcb3a98cffd9af6ea39b Vyama vyakabidhiwa wapigakura

Fri, 16 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

TUME ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imekabidhi kwa vyama vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu nakala tepe ya Daftari la Kudumu la Wapiga kura, orodha ya vituo vya kupigia kura, mfano wa karatasi ya kupigia kura kwa nafasi ya urais, na makamu na jalada la nukta nundu.

Aidha, wakati ikivitaka vyama hivyo kuendelea kuzingatia taratibu na kanuni za uchaguzi, imesema asilimia kubwa ya vifaa vya Uchaguzi Mkuu zimeshawasili nchini na vingi zimeshafika majimboni na vichache vilivyosalia vitawasili nchini wiki hii na kusambazwa ndani ya wakati katika vituo vya kupigia kura.

Hayo yalibainishwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi wa Uchaguzi wa NEC, Dk Wilson Mahera wakati akikabidhi nakala hizo kwa wawakilishi wa vyama 15 vya siasa vinavyoshiriki Uchaguzi Mkuu na kusema katika uchaguzi wa mwaka huu, jumla ya vituo vya kupigia kura vitakuwa 80,155 kwa Tanzania Bara.

Dk Mahera alisema makabidhiano hayo ni kwa mujibu wa Kanuni ya 37 ya Kanuni za Uboreshaji wa Daftari la Kudumu la Wapiga Kura za Mwaka 2018 ambayo inaeleza tume kuvipaia vyama vya siasa nakala ya vitu hivyo kwa ajili ya utambuzi wa wapiga kura wanaoingia katika kituo cha kupiia kura.

“Tumetekeleza Kanuni ya 37 ya Uboreshaji wa Daftari la Wapiga Kura, hivyo vyama vinaweza kupitia taarifa zote za wapiga kura na kuwatambua, sasa wale tunaosikia wanakusanya vitambulisho vya wapiga kura kufanya udanganyifu wataumbuka, kwa sababu mawakala wa vyama watakaoidhinishwa watakuwa na nakala ya daftari hilo la majina na taarifa za wapiga kura wa eneo husika, udanganyifu hautakuwepo,” alisema Dk Mahera.

Alivitaka vyama na wagombea wao wote kuhakikisha kwa siku chache zilizosalia wanaendelea kutii na kuheshimu sheria kwa kufanya kampeni za kistaarabu na kujiepusha na vitendo vya uvunjifu wa amani sambamba na kuwataka kuhamasisha wananchi kujitokeza kupiga kura.

Akizungumzia vituo vya kupigia kura, alisema vipo 80,155 Tanzania Bara huku vituo vya kupigia kura kwa upande wa Zanzibar vitatumia vilivyopo na kuwa NEC inaendelea na maandalizi ya kuviboresha vituo vya wazi kwa kuweka mapaa ili kuhakikisha vinakuwa katika hali bora na kukabiliana na changamoto za hali ya hewa.

Kuhusu jalada la maandishi ya nukta nundu kwa wapiga kura wasioona wenye kujua kusoma maandishi hayo, alisema kwa mara ya kwanza NEC imeandaa karatasi hizo maalumu kwa kundi hilo ili kutoa fursa kwa waliojiandikisha kupiga kura kwa uhuru na uhakika zaidi.

Alisema katika karatasi hizo zina mtiririko wa majina ya wagombea na vyama vyao ili kuwasaidia kushiriki kwa uhuru na kupiga kura wenyewe kwa uhakika na kwamba kwa wale wasioweza kusoma maandishi hayo, wanaruhusiwa kwenda na mtu aliyemchagua anayemuamini.

Kuhusu mawakala wa vyama vya siasa, alisema ni wajibu wa vyama hivyo kupeleka majina ya mawakala wao siku saba kabla ya siku ya uchaguzi ili kuhakikiwa na kuapishwa na kuvitaka vyama vya siasa kupuuza taarifa zilizotolewa na baadhi ya wasimamizi wa uchaguzi za kuvitaka vyama kupeleka majina hayo wiki hii.

Akijibu ombi la Mkurugenzi wa Ufuatiliaji na Tathmini wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), Dk Robert Bujiku, alisema NEC itatoa nakala ya barua za uteuzi wa mawakala kwa msimamizi wa kituo endapo amegoma kumwapisha wakala kwa kisingizio cha kutopata baua, ili kuhakikisha hakuna visingizio visivyo na msingi vitatolewa kukwamisha mchakato huo wa uchaguzi na kuvitaka vyama hivyo kutoa ushirikiano hadi mwisho wa uchaguzi.

Wakishukuru kwa niaba ya wasioona, Mwenyekiti wa Kamati iliyoandaa karatasi za kupigia kura kwa maandishi ya nukta nundu, Jonas Lubago alisema hiyo ni fursa njema kwao kwani ina faida nyingi ikiwemo kupiga kura bila usaidizi,kuwa na hakika ya anayempigia kura na usiri wa kura.

Chanzo: habarileo.co.tz