Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vyama vya upinzani vyashindwa kushiriki uchaguzi Ludewa

IMG 20220822 WA0003 Vyama vya upinzani vyashindwa kushiriki uchaguzi Ludewa

Mon, 22 Aug 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA) pamoja na ACT Wazalendo vyenye uwakilishi wa Madiwani wilayani Ludewa, vimeshindwa kupeleka majina ya wagombea wa nafasi ya makamu mwenyekiti wa halmashauri hiyo kutokana na sababu mbalimbali na kumwezesha mgombea wa CCM kupita bila kupingwa huku wakiahidi kutoa ushirikiano.

Akitoa mwongozo wa uchaguzi Mkurugenzi mtendaji wa wilaya ya Ludewa Sunday Deogratias amesema, awali alitoa taarifa kwa maandishi kuvitaka vyama vitatu vya siasa vyenye wawakilishi kwenye baraza la madiwani wilayani humo kuwasilisha jina la kiongozi atakae wawakilishi kwenye kinyang'anyiro cha makamu mwenyekiti wa halmashauri.

"Nilitoa taarifa kwa maandishi kuwataka CCM, Chadema na ACT Wazalendo kuleta jina la mtu atakaye wawakilisha katika uchaguzi wa makamu mwenyekiti wa halmashauri, lakini mpaka muda unaisha nilipokea jina moja kutoka CCM," amesema Sunday Deogratias.

Kura zilipigwa kwa siri kwa njia ya ndiyo au hapana ambapo wajumbe waliandika kwenye karatasi walizopewa.

Katika uchaguzi huo wajumbe walio piga kura walikuwa 31, mgombea pekee ambaye amekiwakilisha CCM, Leodgar Mpambalyoto, ameibuka mshindi kwa kura 29 za ndiyo, hapana moja na iliyo haribika moja.

Hata hivyo, Diwani wa kata ya Lupingu kupitia Chadema, Jackson Mwakenja alipoulizwa na Mwananchi sababu za kutopeleka jina, amesema wameridhishwa na Makamu Mwenyekiti aliye pita na watamuunga mkono.

“Mimi sikuona umuhimu wa kupeleka jina kwasababu huyu aliye gombea anafaa na alikuwa makamu hata awamu iliyopita anaonesha ushirikiano vizuri kwa sisi madiwani hana shida, mimi nitamuunga mkono kwa moyo wote." Amesema.

Kwa upande wa Diwani wa kata ya Ruhuhu kupitia chama cha ACT Wazalendo, amesema walikuwa hawana taarifa.

"Sisi tulikuwa hatuna taarifa Kama wamepeleka barua kwenye ofisi yetu japo kuwa wao wanadai imepelekwa, ila kiongozi aliyepita yupo vizuri nami nitamuunga mkono," amesema Haule

Chanzo: www.tanzaniaweb.live