Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vyama vya siasa uso kwa uso na kikosi kazi cha Samia

42e5f6d82faa0e173e1cd585e204ed00 Vyama vya siasa uso kwa uso na kikosi kazi cha Samia

Mon, 23 May 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Vyama vya Siasa nchini vinaanza kutoa maoni kwenye Kikosi Kazi cha Rais Samia Suluhu Hassan kinachofanyia kazi masuala yanayohusu demokrasia ya vyama vingi vya siasa kuanzia leo hadi Mei 31 mwaka huu mkoani Dar es Salaam ambapo Chama cha ACT-Wazalendo kitaanza.

Taarifa hiyo iliyotolewa jana na Msajili wa Vyama vya Siasa na kusainiwa na Katibu wa Kikosi Kazi, Sisty Nyahoza ilionesha kuwa kila chama kitakuwa na saa moja kutoa maoni na kwamba siku ya leo vyama vinne vitashiriki.

Vyama hivyo mbali na ACT Wazalendo ni Chauma, NCCR-Mageuzi na UDP. Kesho vyama vitakavyotoa maoni ni CUF, CCM, CHADEMA na TLP huku Mei 25 vyama vya ADA-Tadea, ADC, AAFP na UPDP vitapata nafasi.

Ratiba hiyo inaonesha kuwa Mei 27 vyama vitakavyoshiriki ni Demokrasia Makini, SAU huku Mei 30 ikihusisha vyama vya UMD, CCK, NLD na NRA na mwisho itakuwa Mei 31 ambapo vyama vitakavyohusika ni DP pekee.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotumwa katika vyombo vya habari, kuna maeneo tisa yatakayotolewa maoni ambayo ni pamoja na mikutano ya hadhara na ya ndani ya vyama vya siasa, masuala yanayohusu uchaguzi na mfumo wa maridhiano ili kudumisha haki, amani, utulivu na umoja wa kitaifa.

Maeneo mengine yaliyoainishwa ni pamoja na ushiriki wa wanawake na makundi maalumu katika siasa na demokrasia ya vyama vingi vya siasa, elimu ya uraia, rushwa na maadili katika siasa na uchaguzi, ruzuku ya serikali kwa vyama vya siasa, uhusiano wa siasana mawasiliano kwa umma na katiba mpya.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live