Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vyama vya siasa 13 kuhamasisha Sensa nchi nzima

Vyama Pic Vyama vya siasa 13 kuhamasisha Sensa nchi nzima

Wed, 10 Aug 2022 Chanzo: Mwananchi

Umoja wa vyama vya siasa 13 ambavyo havina uwakilishi bungeni nchini Tanzania, umetangaza kuanza kampeni ya kuzunguka nchi nzima kuhamasisha wananchi kushiriki Sensa ya Watu na Makazi itakayofanyika Agosti 23, 2022.

Mwenyekiti wa Umoja huo, Abdul Mluya amesema wataanza kampeni hiyo jijini Dar es Salaam wakipita mtu kwa mtu, nyumba kwa nyumba na mtaa kwa mtaa ili kuwafikia wananchi wote.

“Tutatangaza tarehe rasmi ya kuanza kampeni hii, suala la sensa sio la chama bali wananchi wote. Tunahitaji wananchi wajitokeze watoe ushirikiano kwa maofisa wa sensa watakavyofika,” amesema Mluya ambaye pia ni Katibu Mkuu wa Chama cha DP

Katibu Mkuu wa AAFP, Rashid Lai ametoa ombi kwa kamisaa wa sensa kuwapa vitendea kazi vikiwemo vipeperushi mapema ili kuwasaidia katika kampeni yao ya uhamasishaji.

Lai amesema zimebaki siku 12 na kiutaratibu hawaruhusiwi kutengeneza vyakwao ili kufanya kampeni bali wanasubiri ofisi hiyo iwapatie.

“Sisi haturuhusiwi kutengeneza vya kwetu kwa ajili ya sensa, tunatakiwa kutumia vile ambavyo vimeandaliwa na Ofisi ya Sensa, tutakwenda kwa wananchi na kwenye majukwaa tutazungumza tu kisiasa bila kuwa na vitendea kazi maalum,” amesema Lai

Saum Rashid ambaye ni Katibu Mkuu wa UDP aliwataka Watanzania kutoa ushirikiano kwa kutoa taarifa ambazo ni sahihi ili kujua idadi sahihi na kubaini mapungufu ambayo yapo katika jamii.

Chanzo: Mwananchi