Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vyama haviwasaidii Wafanyakazi: CHADEMA

Depositphotos 23353070 Stock Photo Site Manager With Safety Vest.webp Vyama haviwasaidii Wafanyakazi

Mon, 13 Feb 2023 Chanzo: dar24

Mjumbe wa Kamati kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo – CHADEMA, John Heche amesema Viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi wamekuwa hawana msaada kwa Wastaafu, na kuwaacha wakihangaika wasijue hatma yao kwa kutopaza sauti juu ya changamoto za wanachama wao.

Heche ameyasema hayo wakati akiongea na Waandishi wa Habari hii Jana Februari 12, 2013 jijini Dodoma, na kusema watu wengi wamejikuta wakiingia katika matatizo kutokana na kuhangaikia mafao yao bila mafanikio.

Amesema, “ hii nchi hatuna vyama vya Wafanyakazi yaani muda huu wangekuwa wapo barabarani kupinga jinsi Serikali inavyowafanyia badala yake wanaona ufahari kupiga picha na viongozi na kukaa nao meza kuu kwenye mei mosi lakini hawawasemei wastaafu ni ajabu.”

Aidha, Heche ameongeza kuwa kutokana na hali hiyo ni wazi kuwa Wafanyakazi wataacha kuwa waaminifu kwa kutafuta njia mbada za kutengeneza maisha kutokata na kutokuwa na uhakika wa mafao yao pindi wanapostaafu.

Chanzo: dar24