Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vitendo vinaonesha kishindo kikubwa cha JPM Oktoba 2020

Eee9811f2f203d98ebca5aeb52283197 Vitendo vinaonesha kishindo kikubwa cha JPM Oktoba 2020

Wed, 7 Oct 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

KWA mfululizo wa vitendo vinavyotoa sauti, kuonwa na kusikika na kila mmoja na mfululizo wa takwimu zilizoshiba kutokana na mambo aliyoyafanya Rais John Magufuli kwa miaka mitano tu ya uongozi wake vinamfanya takribani kila mwananchi akifi ka kwenye sanduku la kupiga kura Oktoba 28 ampigie kura yeye ili kazi iendelee.

Moja ya mahitaji muhimu ya binadamu ni maji na wengi wanasema maji ni uhai. Ni katika muktadha huo, kumekuwa na kasi kubwa ya utekelezaji wa miradi ya maji 1423 yenye thamani ya shilingi trilioni 1.2 nchi nzima.

Hatua hiyo imefanya sasa upatikanaji wa maji kuongezeka maradufu vijijini kutoka asilimia 47 mwaka 2015 hadi asilimia 70.1 na mijini upatikanaji wa maji ukiongezeka kutoka asilimia 74 mwaka 2015 mpaka asilimia 84 mwaka huu Umoja wa Mataifa (UN) unasema uwekezaji huu mkubwa wa serikali ya awamu ya tano kwenye sekta hii muhimu ya maji imefanya nchi kuokoa takribani Sh trilioni 5.2 ambazo Serikali ingetumia kutibu watu magonjwa yanayosababishwa na kunywa maji yasiyo safi na salama.

Kwenye sekta ya umeme kila mmoja ameshuhudia kwa macho yake mapinduzi ya kihistoria. Kutoka vijiji 2,018 tu vili Uchaguzi. Kwa upande wa CCM wanachama walipewa msisitizo wa kujiandikisha na kuhakiki taarifa zao katika daftari la wapigakura.

Sababu ya tano ni kutokuwa na sera na hivyo kuishia kwa kuenda na matukio. Vyama vya upinzani vimekua vikiendesha kampeni bila sera maalumu.

Hii imepelekea kujikuta wakitaka kuwafurahisha wafuasi wao ambao ni makundi hayo matatu kwa kuwakejeli na kujenga uhasama na vyombo vya ulinzi na usalama.

Kwa mfano, kulisema vibaya jeshi la polisi si jambo lenye afya sana kwao na pia wamekuwa wakiwakejeli na kujenga uhasama na vyombo vya habari-mfano TBC waliwaondoa kwenye mkutano wao.

Kumekuwa na kejeli pia na uhasama kwa wasanii wa kizazi kipya wakiwaita wana njaa. Mambo haya yamekuwa yakikera jamii ya Watanzania ambao wanathamini michango ya vyombo vya habari na wasanii.

Sababu ya sita ni tofauti za kimtizamo kati ya viongozi. Kumekuwepo na tofauti za wazi katika vyama viwili vikubwa vya siasa nchini. Tofauti hizi ni kati ya Tundu Lissu ambaye ni mgombea urais kupitia Chadema na Freeman Mbowe ambae ni mwenyekiti wa Chadema.

Msimamo wa Tundu Lissu kutokana na zuio la kufanya kampeni ulikuwa ni kuendelea na kampeni kibabe lakini Freeman Mboe ambaye ndiye mwenyekiti wa chama akakataa kuendelea na kampeni.

Jambo hili limekigawa chama katika makundi mawili; kundi linalounga mkono uamuzi wa Tindu Lissu na lile linalomuunga mkono Freeman Mbowe. Mtafaruku mwingine ni ndani ya ACT-Wazalendo ambao umeibuliwa na Maalim Seif Sharif Hamad, mgombea urais wa chama hicho Zanzibar.

Yeye bila kupitia vikao rasmi alitangaza kumuunga mkono Tundu Lissu kama mgombea uraisi tofauti na mgombea wa chama chake, Bernard Membe. Tofauti hii inatengeneza ufa ndani ya ACT-Wazalendo kwa pande zote mbili za muungano, Zanzibar na Tanzania bara.

Hivyo kumpunguzia idadi ya wafuasi Maalim Seif kutokana na usaliti ndani ya Chama. Kutokana na mambo yaliyoainishwa hapo juu, ni wazi kuwa vyama vya upinzani vinaweza nufaika kwa njia moja tu katika uchaguzi unaotarajiwa kufanyika Tarehe 28 Oktoba 2020 mbayo ni kujifunza na kufanya maandalizi ya uchaguzi wa mwaka 2025.

Makala haya yalichapishwa kwa mara ya kwanza kwenye mtandao wa Jamii Forum jana. MAKALA vyokuwa na umeme tangu tupate uhuru na alivyovikuta mwaka 2015, leo kwa miaka 5 tu Rais Magufuli ameshapeleka umeme mpaka zaidi ya vijiji 9,570 na kubakiza vijiji chini ya 2,500.

Hii imefikisha asilimia 85 ya vijiji vyenye umeme kutoka chini ya asilimia 35 mwaka 2015 na kuifanya nchi ya Tanzania kuwa nchi ya kwanza Afrika kwa usambazaji mkubwa wa umeme vijijini.

Hii imechangiwa na uamuzi wa Serikali ya Rais Magufuli kupunguza kwa zaidi ya asilimia 60 gharama ya kuunganisha umeme kutoka shilingi 177,000 mwaka 2015 mpaka Sh 27,000 tu, jambo lililowafanya Watanzania wengi hata wenye vipato vya chini kabisa kuunganisha umeme.

Hii inaifanya Tanzania kupita maoteo ya Benki ya Dunia (WB) ambayo yalikadiria suala la umeme kwa wote kufikiwa kwenye karne ya 22 kwenye mwaka wa 2101 lakini kwa kasi hii ya Rais Magufuli ambaye ameshasema mpaka kufikia mwaka 2025 vijiji vyote nchini vitakuwa na umeme hivyo kufika kwenye maoteo ya Benki ya Dunia kabla hata ya muda wake wa takriban miaka 75 ijayo.

Hii inaendana na Tanzania kuongoza kwa bei nafuu ya umeme kwa kaya kwa ukanda mzima wa Afrika Mashariki ambapo Tanzania inauza uniti 1 kwa senti 10, Uganda senti 18, Kenya senti 21 na Rwanda senti 26.

Yote haya yanafanikiwa kwa sababu ya Serikali ya Rais Magufuli imeweka misingi mizuri ya usimamizi wa fedha ikiwemo kupambana na vitendo vya rushwa, ufisadi, ubadhirifu na uzembe.

Ni katika muktadha huo, Jukwaa la Uchumi duniani (WEF) kwenye ripoti yake ya mwaka 2019 iliitaja Tanzania kuwa nchi ya 28 duniani kwa usimamizi madhubuti wa fedha na kuziacha nchi majirani na nyingine kubwa duniani kwa mbali sana.

Kenya wakiwa nafasi ya 70, Botswana 37, Msumbiji 69, Uganda 100 na Malawi 106. Hii inathibitika pia kwa namna watu walivyo na imani kubwa na Serikali yao kwa kupambana na rushwa, Taasisi ya Kimataifa ya Uwazi ya Transparency International (Global Africa Corruption Barometer ya 2019) ilisema asilimia 72 ya wananchi wana imani na Rais Magufuli katika vita dhidi ya ufisadi kulinganisha na asilimia 13 tu ya Watanzania ambao mwaka 2015 ndio pekee walikubali nchi yao kupambana na ufisadi.

Usimamizi huu mzuri wa rasilimali fedha ndio umeifanya Tanzania kuwa na uwezo mkubwa wa kutekeleza kwa fedha zake yenyewe za ndani miradi mikubwa ya kimkakati kama Ujenzi wa Bwawa la Umeme la Mwalimu Nyerere linalogharimu Sh trilioni 6.5, ujenzi wa reli ya kisasa (SGR) kwa gharama ya Dola za Marekani bilioni 1.92.

Tusisahau mafanikio kayika utoaji wa elimu bila malipo kwa sababu fedha zote zilizokuwa zinaliwa na mafisadi zimekombolewa kwa kudhibiti wizi, ubadhirifu, ufisadi na matumizi yasiyo ya lazima.

Kwa kutoa elimu bila malipo, Serikali imeshatumia takribani shilingi trilioni 1.01. Hatua chanya imesababisha idadi ya wanafunzi wanaojiunga na darasa la kwanza kuongezeka kutoka wastani wa wanafunzi milioni 1 mpaka milioni 1.6, jambo lililookoa mamia kama si malaki ya watoto wa maskini ambao walikuwa wanakosa fursa ya kupata elimu.

Eneo la afya ambalo ni la msingi sana katika kujenga Taifa lenye ustawi, Serikali imeshajenga vituo 1,769 vya kutolea huduma ya afya zikiwemo zahanati 1,198, hospitali za wilaya 71, za mikoa 10 na za kanda tatu.

Hii ni pamoja na ujenzi wa hospitali ya rufaa iliyoko Mjini Musoma katika eneo la Kwangawa ambayo ilisimama toka miaka ya 1970.

Serikali pia ilipandisha bajeti ya dawa na vifaa tiba kutoka shilingi bilioni 30 mpaka bilioni 270, kuajiri watumishi 14,479 wa kada za afya na mengine lukuki yaliyofanywa katika kuboresha sekta ya afya.

Mapinduzi haya makubwa kwenye sekta ya afya ndio yaliyolifanya Shirika la Afya Duniani (WHO) kuitaja Tanzania kupunguza maambukizi ya malaria kwa asilimia 50 kutoka asilimia 14.2 mwaka 2014 mpaka asilimia saba mwaka 2018.

Kumbuka takwimu nyingi miongoni mwa hizo zinatolewa na hao hao Wazungu wenyewe ambao mapema mwezi Julai mwaka huu Benki ya Dunia iliitangaza Tanzania kuingia uchumi wa kati kutoka nchi maskini kabisa.

Tanzania iliitangazwa na Benki ya Dunia kuingia Uchumi wa kati kwa haraka zaidi kabla hata ya mpango wake wa maendeleo ambao ulikadiria Tanzania kuingia uchumi huo ifikapo mwaka 2025.

Kwa takimwu hizo, bila shaka asiyemkubali Rais Magufuli jina linalomfaa ni ‘mchawi’ Mpaka hapo hujaenda kwenye mapinduzi makubwa yaliyopatikana kwenye miundombinu ya barabara ambapo kwa mara ya kwanza toka Tanzania izaliwe ilipeleka fedha za miradi ya barabara kwenye mikoa na wilaya zote nchini.

Ununuzi wa ndege 11 baada ya kusugua miaka kwa miaka na mindege ya kukodi na mibovu. Hujaenda kwenye mapinduzi mazito yaliyofanyika kwenye madini, utalii, kilimo na kwingine kwingi.

Kwa bahati mbaya ukurasa hautoshi. Mambo ni mengi sana lakini kwa uchache na kwa kumalizia ni eneo la amani na utulivu ambayo ndiyo msingi mkuu wa utekelezaji wa mipango yote ya maendeleo.

Serikali ya Magufuli imeendelea kuweka mkazo katka kuifanya Tanzania kuendelea kuwa kitovu na kisiwa cha amani kote duniani, jambo lililofanya mtandao wa Global Peace Index unaohusika na kupima hali ya amani duniani kuitaja Tanzania kuwa nchi yenye amani na utulivu wa hali ya juu sana Afrika na dunia kwa ujumla.

Ripoti ya mtandao huo ya mwaka 2020 iliitaja Tanzania kuongoza kwa amani na utulivu Afrika Mashariki, huku ikishika nafasi ya sita barani Afrika na ya 52 duniani kote.

Kwa vitendo na takwimu hizi chache tu kati ya nyingi zilizotapakaa kwenye kila sekta inatosha kusema Mitano Tena kwa Dk John Magufuli ili kazi iendelee.

0657475347

Chanzo: habarileo.co.tz