Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi watakiwa kusikiliza, kutatua kero za wananchi

11132 Viongozi+pic.png TanzaniaWeb

Tue, 10 Jul 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zanzibar. Naibu katibu mkuu wa CCM Zanzibar, Abdallah Juma Sadalla Mabodi amewakumbusha viongozi wa majimbo kusikiliza na kutatua matatizo ya wananchi maeneo yao.

Akizungumza na wananchi na viongozi wa majimbo ya Pangawe na Kijitoupele eneo la kwa Mabata Fuoni juzi, Mabodi alisema wananchi wanawachagua viongozi ili kuwasaidia kutatua matatizo yanayowakabili.

Mabodi alisema kwamba wananchi wanakabiliwa na matatizo ya huduma za jamii, hivyo ni vyema viongozi hao kuelekeza nguvu zao kwa wapigakura wao.

Naye mwakilishi wa Pangawe, Khamisi Juma Mwalimu alisema kwamba kutokana na ukosefu wa maji safi na salama, ameamua kuwachimbia kisima wakazi wa eneo hilo.

Chanzo: mwananchi.co.tz