Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi wastaafu wasimulia ujasiri, uimara wa Ndejembi

34401 Pic+ndejembi Tanzania Web Photo

Tue, 1 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mkurugenzi mtendaji wa Taasisi ya Mwalimu Nyerere,  Joseph Bujiku ameeleza maisha ya mwanasiasa mkongwe nchini Tanzania, Pancras Ndejembi kuwa yalijaa uvumilivu na ukweli mbele za watu, alikuwa shujaa aliyemueleza ukweli Mwalimu Julius Nyerere.

Ametoa kauli hiyo leo Jumanne Januari Mosi, 2019 katika salamu zake za rambirambi muda mfupi kabla ya mazishi ya mwanasiasa huyo mjini Dodoma.

Ndejembi alifariki dunia Jumamosi Desemba 29, 2018  katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma alikopelekwa baada ya hali yake kubadilika ghafla.

Akieleza anavyomfahamu marehemu, Butiku amesema alimfahamu mwanasiasa huyo wakati akiwa katibu wa rais.

"Mimi nilikuwa katibu wa mwalimu na huyu mzee alikuwa akimfuata mwalimu kumwambia ukweli bila hofu, lakini kikubwa alikuwa mvumilivu," amesema Butiku.

Amesema amekuwa na amani iliyopitiliza moyoni mwake kuona Ndejembi amekufa akiwa na msimamo wake usioyumba.

Mwanasiasa mwingine mkongwe nchini Tanzania, Hassan Nasoro Moyo amesema kuwa walifanya kazi na marehemu na alikuwa mtu mwenye msimamo, hakusita kumueleza ukweli Mwalimu Nyerere.

Moyo amesema enzi za uhai wake, Ndejembi alikuwa jabali la siasa na mipango yake haikuwahi kufeli siku zote, kwamba walimtumia katika maeneo mengine kufikisha ujumbe.

Naye balozi mstaafu, Job Lusinde amesema alikutana na marehemu mwaka 1955 wakiwa walimu na walikubaliana kuacha kazi na kuingia katika siasa kumsaidia Mwalimu Nyerere katika harakati za kudai uhuru.

Lusinde amesema katika kipindi chote urafiki wao haukuwahi kupungua na alimtembelea Ndejembi siku moja kabla ya kifo chake.



Chanzo: mwananchi.co.tz