Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi waaswa kusikiliza kero za wananchi

Viongozi Waaswa Kusikiliza Kero Za Wananchi Viongozi waaswa kusikiliza kero za wananchi

Mon, 6 Feb 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma, na Mjumbe wa Halmashauri kuu Taifa Bi, Leila Ngozi ametoa rai kwa viongozi wa serikali kuendelea kutenga muda kwa ajili kusikiliza na kutatua changamoto za wananchi.

Wito huo umetolewa wakati wa kumbukumbu ya miaka 46 ya Chama cha mapinduzi iliyofanyika katika kata ya Ipera Halmashauri ya Wilaya ya Mpwapwa Jijini Dodoma tarehe 5/02/2023.

Mlezi wa Chama cha Mapinduzi Bi, Leila ameomba viongozi kuendelea kutekeleza ilani ya Chama Cha Mapinduzi ambayo wanaccm wanajivunia imefanya mambo mengi.

Ameongeza kusema Ilani imeelekeza katika sura ya 10 ibara ya 251, “kuwa tunatakiwa tutenge muda wakwenda kusikiliza wananchi wetu, Niwaombe wananchi tuendelee kueleza changamoto zetu kwa viongozi wetu ili waweze kuzifanyia kazi,” alisema Bi, Leila.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Mkoa wa Dodoma Alhaji Adam Kimbisa ametoa rai kwa watendaji wa Serikali kutenda haki katika maamuzi na kuepuka dhuluma na uonevu.

“Wanachi toeni taarifa kama kuna mienendo isiyofaa kwa watendaji wa serikali katika kutoa huduma,” alisema Alhaj Kimbisa

Awali Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe, Rosemary Senyamule amesema ilani ya Chama cha Mapinduzi inatekelezeka kwa kasi kubwa kutokana na dhamira ya dhati ya Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi Taifa ambaye pia Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.

“Upo mradi mkubwa wa umwagiliaji ambao upo katika hatua nzuri ya ujenzi, na mradi wa ukarabati wa Hospitali ya wilaya ya Mpwapwa ambao umeshakamilika na Mheshimiwa Rais ameridhia ujenzi wa barabara ya lami ili kuunganisha barabara wilaya ya Mpwapwa kwa lami,” alisema Mkuu wa Mkoa.

Naye Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera Bunge na Uratibu (Mb) wa Kibakwe Mhe. George Simbachawene amesema furaha ya watu wa Ipera ni kukamilika wa kituo cha afya cha Ipera.

“Tunajivunia maendeleo lakini lazima tuendele kufanya kazi na tujitegemee katika kujenga taifa,” alisema waziri Simbachawene.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live