Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi Chadema wahojiwa polisi, wadaiwa kufanya vurugu gerezani

98992 Pic+wahojiwa Viongozi Chadema wahojiwa polisi, wadaiwa kufanya vurugu gerezani

Fri, 13 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Kamanda wa Polisi Wilaya ya Ilala, Zuberi Chembela amesema viongozi wa Chadema wanashikiliwa katika kituo cha polisi Stakishari kwa mahojiano kwa madai ya kufanya vurugu katika gereza la Segerea jijini Dar es Salaam.

Kati ya wanaoshikiliwa ni mwenyekiti wa Baraza la Wanawake la Chadema (Bawacha), Halima Mdee ambaye pia ni mbunge wa Kawe; mbunge wa Bunda, Ester Bulaya; Meya wa Ubungo, Boniface Jacob; katibu wa Chadema Mkoa wa Dar es Salaam, Henry Kileo; diwani wa Tabata, Patrick Asenga na mjumbe wa baraza la Vijana Chadema (Bavicha), Hadija Mwago.

Wakati Chembela akieleza hayo, naibu katibu mkuu wa Chadema (Bara), Benson Kigaila amelieleza Mwananchi leo kuwa takribani wanachama 16 wanashikiliwa na polisi.

Katika ufafanuzi wake Chembela amesema watuhumiwa hao walikwenda katika gereza la Segerea na kukuta geti limefungwa lakini walilazimisha kuingia ndani licha ya kuzuiwa na askari wa Jeshi la Magereza.

“Jambo hilo liliwafanya askari Magereza kuwadhibiti, kuwaweka chini ya ulinzi na waliwafikisha kituo cha polisi Stakishari ambako wapo wanahojiwa,” amesema Chembela.

Amebainisha kuwa dhamana kwa viongozi hao waliokwenda katika gereza hilo kumchukua mwenyekiti wa Chadema, Freeman Mbowe aliyetoka jela baada ya kulipa faini ya Sh70 milioni, ipo wazi endapo watatimiza masharti.

Habari zinazohusiana na hii

Advertisement
“Wananchi wawe watulivu kwa amri halali zinazotolewa na vyombo vya ulinzi na usalama. Si jambo la kiungwana umekuta geti limefungwa halafu badala ya kupiga hodi unalazimisha kupita. Hata wewe ingekuwa kwako ungekubali.” Amehoji.

Katika maelezo yake Kigaila amedai, “Mbali na wanachama 16 kukamatwa wengine wanne wameumizwa  baada ya kuibuka mvutano kati yao na askari Magereza.”

Hadi leo saa 1:00 ushiku viongozi hao pamoja na wanachama wengine walikuwa wakiendelea kuhojiwa katika kituo cha Polisi Stakishari.

Chanzo: mwananchi.co.tz