Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

TV

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi CHADEMA wajiunga ACT- Wazalendo

Actpiic Viongozi CHADEMA wajiunga ACT- Wazalendo

Sat, 25 Jun 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Viongozi na wanachama wa Umoja wa Wanafunzi wa Vyuo Vikuu na Vyuo vya Kati wa Chadema (Chaso) wa Chuo kikuu cha Dar es Salaam wamejiunga na chama cha ACT wazalendo.

Jumla ya wanachama 23 wa jumuiya hiyo wamepokelewa na Katibu Mkuu wa chama hicho, Ado Shaibu pamoja na katibu wa Ngome ya vijana, Mwanaisha Mndeme.

Akizungumza leo Jumamosi Juni 25, 2022 na aliyekuwa Makamu Mwenyekiti na Mratibu wa Chaso UDSM, Abdul Carter amesema wamechukua uamuzi huo kwa kuwa ACT Wazalendo ni chaguo sahihi kwa kuwa ni chama kinachokuwa kwa kasi.

Mafanikio yaliyopatikana ndani ya chama hicho kwa miaka nane ni makubwa ukilinganisha na vyama vingine vilivyokuwepo kwenye ulingo wa siasa kwa zaidi ya miaka 30.

ACT Wazalendo inatoa mwongozo wa kisiasa katika kuelekea mabadiliko ya katiba mpya, lazima tupate tume huru ndio tupate Katiba Mpya. Tunaamini ipo siku nchi hii itaongozwa na Chama cha ACT, “ amesema Carter.

Ameeleza kuwa sababu za kujiondoa Chaso iliwaendelee na maono yao ya kujikita katika kwenye harakati zanye malengo ya kuikombo jamii.

"Tumejiridhisha kuwa ACT Wazalendo ndio chama sahihi cha kupigania maono yetu ya kisiasa, kijamii na kiuchumi, tumejiridhisha kuwa hiki ni chama kinachowalea vijana kiuongozi ili watimize ndoto zao na ndoto za jamii," amesema Carter.

"Tumefurahia msimamo wa ACT Wazalendo wa kupigania Tume Huru ya Uchaguzi kuelekea katiba mpya, hivyo tunaamini Act itatupa jukwaa pana zaidi la kupigania Tume huru ya uchaguzi na katiba Mpya, " amesema Carter.

Pia, amesema Chaso walipuuzia wazo lao la kufungua kesi ya kikatiba ili kudai marekebisho ya sheria ya Vyuo vikuu pamoja na kanuni zake ambayo inatoa katazo kwa wanachuo kujihusisha na siasa katika mazingira ya Chuo na makazi ya wanafunzi.

Hivyo wanawashukuru ACT Wazalendo kwa kuwapokea vizuri na watashirikiana na chama katika kujenga ushawishi wa chama katika vyuo vikuu nchini.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live