Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi CCM Tanga mzilee Jumuiya

Viongozi CCM Tanga Mzilee Jumuiya.jpeg Viongozi CCM Tanga mzilee Jumuiya

Thu, 5 Oct 2023 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Umoja wa vijana wa Mkoa wa Tanga ndugu Ramadhan Ally Omary (Somo) amewakumbusha Viongozi wa CCM wa Wilaya za Mkoa wa Tanga na ngazi zote za chini kuhakikisha wanashirikiana na Jumuiya za Chama zote tatu, ili kuweza kuzisimamia na kuhakikisha zinafanya kazi iliyo bora.

Alisema “nasi viongozi wa Jumuiya tukibebwa basi tujishike, tukishikiliwa na sisi tung'ang'anie ili Viongozi wa Chama wasichoke kutulea”.

Alisisitiza kuwa kuna umuhimu wa Chama na Jumuiya kushirikiana katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi serikali za mitaa 2024 na Uchaguzi Mkuu 2025 ili kuiwezesha CCM kupata kura nyingi na kuendelea kushika dola.

Pamoja na hayo ndugu Ramadhan Omary katika kuhamasisha michezo kwa vijana, alitoa mipira mitano katika Tarafa ya Bwembwela iliyopo katika Wilaya ya Muheza kwa lengo ya kuanzishwa kwa ligi ya vijana ya mpira wa miguu ambayo alielekeza iitwe Ligi ya Mama Samia

Chanzo: www.tanzaniaweb.live