Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi ACT wajadili nidhamu ya wagombea

62bf7b85cfae2eea206a03064819b3a0 Viongozi ACT wajadili nidhamu ya wagombea

Mon, 24 Aug 2020 Chanzo: habarileo.co.tz

CHAMA cha ACT-Wazalendo kimesema siku yoyote kuanzia leo kitatoa taarifa kuwa lini watazindua kampeni, Ilani ya Uchaguzi na kuweka wazi suala la ushirikiano baina yao na vyama vingine vya siasa vya upinzani katika uchaguzi mkuu unaoanza kampeni kesho kutwa.

Akizungumza na gazeti hili jana kwa njia ya simu jijini Dar es Salaam, Naibu Katibu wa Habari, Uenezi na Mawasiliano ya Umma, wa chama hicho, Janeth Rithe alisema jana kuwa hivi sasa viongozi wa chama na kamati wanashughulikia mashauri yaliyojitokeza kuhusu wagombea.

“Kamati husika zinaendelea kushughulikia mashauri ya kinidhamu ndani ya chama kwa mashauri ya wagombea waliyoletwa, lakini mashauri mengi tumeyapatia ufumbuzi na tayari wagombea tuliowapitisha tumewapa barua kwenda Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC), na kuhusu ushirikiano wetu na vyama vingine tutatoa taarifa hivi punde”alisema Janeth.

Wiki iliyopita Kiongozi Mkuu wa chama hicho, Kabwe Zitto alisema Watanzania hawatavisamehe vyama vya siasa vya upinzani iwapo havitamsimamisha mgombea mmoja wa urais.

“Watanzania hawatatusamehe iwapo hatutasimamisha mgombea mmoja wa urais, kwenye majimbo tuache ubinafsi tuangalie anayekubalika asimame,Tanzania ni kubwa kuliko vyama vyetu, watanzania wanatana ushirikiano kuleta mabadiliko kwenye uchaguzi huu, joto la uchaguzi mmeliona watu wamechangamka,wanataka ushirikiano na sio ubinafsi,”alisema Zitto.

Alitoa kauli hiyo Dar es Salaam wakati akizungumza na vyombo vya habari muda mfupi baada ya chama hicho kutambulisha viongozi wa kitaifa wa timu ya kampeni kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu.

Chanzo: habarileo.co.tz