Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Viongozi ACT Wazalendo waikera CCM

7b13b6db00b83584de020c58c11b8a76.jpeg Viongozi ACT Wazalendo waikera CCM

Wed, 11 Aug 2021 Chanzo: www.habarileo.co.tz

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM) kimekanusha matamshi yaliyodaiwa kutolewa na viongozi wa juu wa Chama Cha ACT- Wazalendo kuwa Mbunge wa CCM Jimbo la Konde Sheha Mpemba Faki, alijiuzulu kutekeleza uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho.

Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi, Shaka Hamdu Shaka jana alimtaka Makamu Mwenyekiti wa ACT- Wazalendo, Juma Duni Haji na Mjumbe wa Kamati Kuu ya chama hicho, Othman Masoud Othman waache siasa za udanganyifu na upotoshaji.

Shaka alisema CCM ilishangazwa na kilichodaiwa kuwa ni uzushi wa viongozi hao waliodaiwa kusema walikutana na Rais Samia Suluhu kuzungumzia uchaguzi wa Jimbo la Konde.

"Viongozi hao wanapaswa kuacha siasa za mazoea, unafiki, na uzandiki kwa kudanganya wanachama ambao wamekuwa wakihama nao kila wanakokwenda,” alisema.

Aliongeza: "CCM kinalaani na kukanusha vikali siasa za uzushi na uzandiki zinazoanza kufanywa na ACT-Wazalendo kupitia kwa Duni na mwenzake Othman. Waachane na tafsiri batili iliyozoeleka ya kuwaaminisha baadhi ya watu kuwa siasa ni uongo, wakati siasa si uongo kwani ni taaluma inayosomewa na wakapatikana wataalamu huku ikibeba ustawi wa maisha na maendeleo ya watu."

Shaka alisema Kamati Kuu ya CCM haiwezi kuitishwa kujadili ajenda yoyote inayokihusu chama cha ACT-Wazalendo na kwamba, Faki alijiuzulu kwa sababu za kifamilia.

Chanzo: www.habarileo.co.tz