Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vikao vya ngazi ya juu CCM kufanyika Dar es Salaam

63894 Vikaopic

Mon, 24 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam: Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania kinatarajia kufanya vikao vyake Kamati Kuu (CC) pamoja na Halmashauri kuu (NEC) wiki ijayo Dar es Salaam.

Wakati kikao cha kamati kuu vitafanyika Juni 26, 2019 kikao cha NEC kitafanyika Juni 27,2019 na kitakuwa cha kawaida kwa mujibu wa kalenda ya chama na Katiba ya CCM ibara ya 101(2).

Taarifa iliyotolewa kwa vyombo vya habari jana Ijumaa Juni 22, 2019 na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Humphrey Polepole ilisema kikao cha Kamati kuu kikitanguliwa na vikao vya Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa kitakachofanyika Juni 24,2019 na kufuatiwa na semina ya makatibu wa mikoa Juni 25, 2019.

Polepole alisema semina hiyo itaendeshwa na Makamu Mwenyekiti wa chama hicho (Bara), Philip Mangula pamoja na wajumbe wa Sekretarieti ya Kamati kuu ya Taifa.

Taarifa hiyo pia inasema wajumbe wa vikao hivyo watapata fursa ya kutembelea miradi ya kimkakati inayotekelezwa na Serikali ya CCM ya awamu ya Tano iliyo katika mikoa ya Dar es Salaam na Pwani.

 

Pia Soma



Chanzo: mwananchi.co.tz