Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana watakiwa kujitokea kugombea uongozi CCM

JYYFYVFFC Vijana watakiwa kujitokea kugombea uongozi CCM

Sat, 9 Dec 2023 Chanzo: Mwananchi

Mwenyekiti wa CCM Wilaya ya Mtwara Vijijini, Nashiri Pontiya amewahamasisha vijana kujitokeza kugombea nafasi za uongozi ndani ya chama hicho, badala ya kukubali kukatishwa tamaa.

Pontiya ametoa kauli hiyo leo Desemba 9, 2023 katika sherehe za maadhimisho ya miaka 62 ya uhuru wa Tanzania Bara, huku akiwaonya vijana kuacha kutumika kukashifu viongozi.

Amesema kuwa ni vema vijana wakafanya mambo yatakayowafanya waaminike na kupewa nafasi mbalimbali za uongozi.

“Vijana tuwanie nafasi za uongozi ndani ya CCM, tuache woga tuwe na uthubutu. Wakati mwingine vijana wanakatishwa tamaa ili wasigombee.

“Hizi nafasi tukumbuke wapo waliokuwepo wakatoka na sisi tutatoka wataingia wengine,” amesema.

Naye Naibu Meya wa Manispaa ya Mtwara Mikindani, Sixmund Lungu amesema kuwa miaka 62 ya uhuru inatosha kuonyesha wapi waasisi wao walipoanzia na wao wako wapi.

“Katika maadhimisho haya ni sehemu ya kukumbushwa wapi tulipo na tunayaona mafakio huko tundako, tumeshuhudia maendeleo makubwa ambayo nchi yetu imepiga,” amesema Lungu.

Chanzo: Mwananchi