Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana msitumike kupasua chama- Samia

Samia Leo Zanz.jpeg Samia Suluhu Hassan, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania

Fri, 7 Jan 2022 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Rais Samia Suluhu Hassan amewataka vijana wa chama cha Mapinduzi kutokubali kutumiwa kusababisha mpasuko ndani ya chama hicho.

Akizungumza wakati wa maandamano ya maadhimisho ya miaka 58 ya Mapinduzi y Zanzibar, Samia amesema kuwa vijana wote walio ndani ya cham a hicho wanapaswa kuwa mstari wa mbele kulinda na kusimamia ilani ya CCM.

"Msitoe fursa kutumiwa kukipasua chama. Jeuri yenu, majidai yenu, kwenda kwenu kifua mbele ni kwa sababu chama kiko imara." - Rais Samia Suluhu Hassan akizungumza katika Maadhimisho ya Kilele cha Matembezi ya Miaka 58 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live