Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Vijana Chadema wamchukulia Mbowe fomu agombee uenyekiti

85846 Pic+mbowe Vijana Chadema wamchukulia Mbowe fomu agombee uenyekiti

Tue, 26 Nov 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Vijana wa chama kikuu cha upinzani nchini Tanzania cha Chadema kutoka maeneo mbalimbali wamechukua fomu kwa ajili ya kumshawishi Mwenyekiti wa chama hicho, Freeman Mbowe kutetea nafasi hiyo.

Chama hicho kitafanya uchaguzi wa viongozi Desemba 18, 2019 ambapo shughuli ya uchukuaji na urejeshaji wa fomu utahitimishwa Novemba 30, 2019.

Vijana hao walifika makao makuu ya Chadema yaliyopo Ufipa, Kinondoni jijini Dar es Salaam wakiwa wanaimba nyimbo mbalimbali huku wengine wakisikika wakisema ‘Mbowe tuvushe’ ‘mwamba tuvushe.’

Akizungumza leo Jumatatu Novemba 25, 2019 mratibu wa vijana Taifa, Danieli Ngogo amesema baada ya kazi hiyo ya kuchukua fomu hatua itakayofuata ni kumkabidhi Mbowe na kisha kumuomba agombee nafasi hiyo.

Amesema endapo Mbowe atakubali kugombea itafuata taratibu zote kama katiba na kanuni zinavyoelekeza .

"Sisi kama vijana hatuna mgombea tunachofanya ni kuangalia nani anayetufaa tunaenda kumshawishi Mbowe awe mgombea," amesema Ngogo

"Wagombea wengi watajitokeza sisi kama vijana na wanachama tunayo haki ya kumshawishi mtu tunayeona anao uwezo wa kuhimili majaribu kugombea," amesema

Ngogo amesema katika kazi hiyo ya kuchanga fedha limehusisha makundi mbalimbali nchi nzima ambapo jumla ya Sh5.6 milioni zimepatikana.

Mratibu wa mkoa wa Dar es Salaam, Twaha Mwapaya amesema Jumatano Novemba 27, 2019 vijana watamkabidhi fomu hiyo popote atakapokuwepo.

Chanzo: mwananchi.co.tz