Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Video: Upo usemi wa enzi usemao mke wa mfalme hapaswi kuhisiwa amechepuka – Rais Magufuli

335 E92105ea 93dd 418b A5c3 4df658f34d75 TZW

Mon, 18 Dec 2017 Chanzo: bongo5.com

Aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi(CCM) taifa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amesema kuwa Chama hicho hakitamvumilia kiongozi au Mwanachama wa CCM mwenye kutuhumiwa au kujihusisha na vitendo vya rushwa, utapeli, wizi, ubadhilifu huku akitoa mfano kuwa ‘upo usemi wa enzi usemao mke wa mfalme hapaswi kuhisiwa amechepuka’ hivyo basi kama kuna viongozi wa namna hiyo wamechaguliwa wanapaswa kujirekebisha katika chama hicho.

Rais Magufuli amesema hayo leo katika Mkutano Mkuu wa 9 wa CCM unaoendelea mjini Dodoma ambapo pamoja na hayo amesema kuwa Chama hicho hakitamvumilia kiongozi au Mwanachama wa CCM mwenye kutuhumiwa au kujihusisha na vitendo vya rushwa, utapeli, wizi, ubadhilifu , jambazi, ulevi uliopindukia, kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.

“Kiongozi anapaswa kuwa mfano wa kuigwa kwa wanachama na wananchi kwa ujumla haifai kamwe na Chama hakitamvumilia kiongozi au Mwanachama wa CCM mwenye kutuhumiwa au kujihusisha na vitendo vya rushwa, utapeli, wizi, ubadhilifu , jambazi, ulevi uliopindukia, kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya nakadhalika(n.k),” amesema Rais Magufuli.

“Upo usemi wa enzi usemao Mke wa Mfalme hapaswi hata kuhisiwa kuwa amechepuka hivyo basi kama kuna viongozi wa namna hiyo wamechaguliwa ni vyema wakajirekebisha na niwaombe sana ndugu zangu wana – CCM tuyavunje makundi yote tuliyoyaanzisha kwakati wa uchaguzi kwasababu wakat wa kampeni umekwisha sasa tunatakiwa tuchape kazi ili kukiimarisha zaidi chama chetu,” ameongeza. 

Chanzo: bongo5.com