Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Wazee Chadema wawazulia jambo wabunge CCM

Wed, 9 Jan 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es salaam. Baraza la Wazee la Chadema limewafananisha wabunge wengi wa CCM na kasuku kwa maelezo kuwa hawachukui jukumu la kukemea udhaifu wa masuala mbalimbali wanapokuwa bungeni.

Wakati wazee hao wakieleza hayo, mbunge wa Mbagala (CCM), Issa Mangungu amepinga kauli hiyo, akibainisha kuwa wabunge wa chama hicho tawala wapo makini na wanatekeleza majukumu yao kwa ajili ya wananchi na Taifa.

Kauli hiyo ya wazee wa Chadema imetolewa leo Jumatatu Januari 7, 2019 na na mwenyekiti wa baraza hilo, Hashim Issa Juma akihusisha mazingira ya wabunge hao kukosa uhuru wa kukemea udhaifu ndani ya Bunge na badala yake wamekuwa wakibadilika badilika.

Katika ufafanuzi wake kuhusu ukasuku wa wabunge hao, Juma amesema wabunge hao ndiyo waliopongeza udhaifu uliokuwa kwenye mabadiliko ya kikokotoo cha mafao ya wastaafu, lakini baada ya Rais Magufuli kurejesha utaratibu wa zamani, walipongeza.

Amesema wabunge hao wa CCM ndio waliopitisha sheria nyingi dhaifu zikiwamo za madini lakini leo wamempongeza Rais Magufuli kwa kuagiza mabadiliko ya sheria. 

Katika maelezo yake Mangungu amesema kila chama kina umoja wa wabunge wao, akisema endapo kanuni za mabadiliko ya kikokotoo yangewekwa wakati wa vikao vya Bunge, mbunge binafsi angekuwa na uwezo wa kutoa hoja binafsi.

Amesema wabunge hao wamekuwa wakitekeleza wajibu wao kama sheria na kanuni za Bunge zinazoelekeza.

Kuhusu hoja ya kupitisha sheria na baadaye zinatenguliwa na Rais Magufuli, Mangungu alitolea mfano wa sheria za gesi na madini.

“Sheria za madini na gesi zilipitishwa kwa hati ya dharura kwa malengo maalumu, baada ya malengo kufanyiwa kazi zikaletwa tena ili kurekebishwa kwa sababu tayari yale malengo yalikuwa yameshatimizwa,” alisema  Mangungu huku akikataa kuweka wazi malengo hayo.



Chanzo: mwananchi.co.tz