Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Wabunge Chadema wasota rumande

Tue, 26 Feb 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Morogoro. Wabunge wawili wa Chadema, Suzan Kiwanga (Mlimba) na Peter Lijualikali (Kilombero) na wenzao saba wamefikishwa mahakamani na baadaye kurudishwa rumande hadi Machi Mosi Mahakama itakaposikikiliza ombi la kupinga dhamana yao lililowasilishwa na upande na mashtaka.

Washitakiwa hao mwaka jana walipofikishwa mahakamani kwa mara ya kwanza walikuwa 13 na kusomewa mashtaka nane likiwemo la kuchoma moto ofisi ya Serikali ya kijiji cha Sofi wilayani Malinyi.

Hata hivyo Mahakama iliwaachia huru baada ya upande wa mashtaka kushindwa kuwasilisha ushahidi wa kutosha ili kuwatia hatiani kabla ya Serikali kufufua tena kesi hiyo.

Jana mbele ya hakimu mkazi mfawidhi mkoa wa Morogoro, Elizabeth Nyembele wakili wa Serikali, Edger Bantulaki aliwasilisha ombi la kupinga dhamana ya washtakiwa hao kutokana na baadhi ya washtakiwa hawajapatikana hivyo dhamana inaweza kukwamisha upatikanaji wa washtakiwa wengine.

Wakili wa utetezi, Josephine Jackson alisema: “Baada ya kupata pingamizi tutawasilisha majibu ya hoja za pingamizi hilo la Serikali na kesi itatajwa tena Machi Mosi.”



Chanzo: mwananchi.co.tz