Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Uteuzi wa wagombea ACT- Wazalendo watangazwa

Video Archive
Sat, 29 Feb 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Kamati Maalumu ya Uchaguzi wa Chama cha ACT- Wazalendo, Omar Said Shabaan amesema hatua inayofuata baada ya mchakato wa kuchukua na kurejesha fomu kukamilika ni mchujo wa wagombea utakaofanyika kati ya Machi Mosi na Machi 2.

Shabaan ametoa kauli hiyo leo Ijumaa Februari 28, 2020 wakati akitoa taarifa ya mwenendo wa uchukuaji na urejeshaji fomu za kuwania nafasi ndani ya chama hicho ambao mchakato ulikamilika Februari 26 baada ya kudumu kwa mwezi mmoja.

"Zaidi ya wanachama 200 kutoka maeneo mbalimbali wamechukua na kurejesha fomu za kuomba uongozi ngazi mbalimbali. Kwa utaratibu wa kanuni za uchaguzi za chama majina haya yatapelekwa kwenye vikao vya uteuzi.

"Kikao cha kwanza kitakuwa ni Kamati Kuu kitakachoketi  Machi Mosi na kuteua majina ya waliongea nafasi zote  za ngome. Kutakuwa na kikao cha halmashauri kuu kitakachofanyika Machi 2 ambacho kitatea na kuchukua majina ya wagombea wote walioomba nafasi ya za kitaifa ndani ya chama hicho,"amesema Shabaan.

Shabaan amesema baada ya majina ya wagombea hao kupitia katika ngazi hizo kitakachofuata ni kampeni za watia nia hao zitakazodumu ndani ya siku saba.

Uchaguzi wa viongozi wakuu utafanyika Marchi 14, ukitanguliwa na chaguzi nyingine za ngome ya wazee, utakaofanyika Machi 7 na Machi 8 ngome ya wanawake.

Pia Soma

Advertisement
Nafasi zinazogombewa katika uchaguzi huo ngazi ya chama hicho Taifa ni pamoja ni kiongozi wa chama, naibu kiongozi, mwenyekiti wa Taifa, makamu mwenyekiti Bara na Zanzibar, katibu mkuu, wajumbe wa Halmashauri Kuu (nafasi 15) na wajumbe wa Kamati Kuu (nafasi nane).

Ngome ya wanawake nafasi zinazogombewa ni mwenyekiti wa ngome, makamu mwenyekiti wa ngome, katibu na wajumbe wa halmashauri kuu(nafasi 15) na wajumbe wa kamati kuu (nafasi nane).

Wakati ngome ya vijana nafasi zinazogombewa ni mwenyekiti, makamu mwenyekiti Bara na Zanzibar, katibu na naibu wake, wajumbe wa halmashauri kuu Taifa na wajumbe wa mkutano mkuu.

Miongoni mwa waliochukua fomu kugombea nafasi mbalimbali katika chama hicho ni pamoja na Maalim Seif na Yeremia Maganja (uenyekiti), Zitto Kabwe na Ismail Jussa  (kiongozi wa chama), Juma Duni Haji (makamu mwenyekiti  Zanzibar), Dorothy Semu  na Riziki  Ngwali (makamu mwenyekiti bara).

Chanzo: mwananchi.co.tz