Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Profesa Lipumba asema hana tatizo na Maalim Seif

Video Archive
Tue, 17 Mar 2020 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha CUF, Profesa Ibrahim Lipumba ameeleza kuwa hana tatizo lolote na aliyekuwa katibu mkuu wa chama hicho, Maalim Seif.

Profesa Lipumba ameeleza kushangazwa kwake na kile anayoiita chuki ya wazi inayoonyeshwa na kwake na Maalim.

“Mimi namtakia heri huko alikokwenda ila sioni kwamba mawazo yake na kiongozi wa chama alichokwenda kama yanaendana,”

“Binafsi sina tatizo naye namstaajabu amejenga chuki na mimi na katika siasa ukijenga chuki namna hiyo huwezi kufanikiwa. Alijenga chuki na Mapalala, amejenga chuki na mimi na huwezi jua uchaguzi ukiisha anaweza kujenga chuki kwa Zitto,”

Kuhusu kuondoka kwa Maalim na wanachama wengine Profesa Lipumba amekiri kuwa iliwapa athari lakini hata hivyo chama hicho kina watu imara walioziba nafasi zilizoachwa wazi.

Chanzo: mwananchi.co.tz