Tabora . Mwenyekiti wa chama cha wananchi CUF Profesa Ibrahim Lipumba amesema mkakati wa kuminya demokrasia unaofanywa na chama tawala na vyombo vya dola ni mkakati wakutaka upinzani kukata tamaa .
Ameyasema hayo leo Oktoba 2,2019 wakati akiongea na viongozi wa wilaya, na wanachama wanaotegemea kugombea nafasi mbalimbali katika uchaguzi wa vijiji, vitongoji na mitaa.
Amesema ni muhimu kila mmoja kufahamu kanuni za uchaguzi kwa kuwa mkakati uliopo ni wagombea kupita bila kupingwa
Mwenyekiti huyo wa Chama cha wananchi CUF amesema ukosefu wa haki umekithiri hadi kwenye taaarifa ya umoja wa mataifa kuhusu hali ya furaha kwa wananchi.
"Tunahitaji mabadiliko kuelekea 2020 ili tuwe nchi ambayo watu wale hawakati tamaa na inakuwa nchi yenye furaha" amesema
Mkurugenzi wa Habari na Mahusiano ya Umma wa CUF Abdul Kambaya amesema kufanya maamuzi sahihi kwa watu au vitu inahitaji kujitambua.
Pia Soma
- Kimbunga kilichoikumba Arusha, Muongoza watalii aliyezama aendelea kusakwa
- Diamond, Tanasha wapata mtoto wa kiume
- Sheria ya kudhibiti 'habari feki' yaanza kutumika Singapore
"Mkoa wenu umepewa bahati ya wazee wenu kupigania uhuru lakini mmepewa mtu anayeheshimika Duniani" amesema Kambaya
Profesa Lipumba anafanya ziara hiyo kuhamasisha uchaguzi wa Serikali za mitaa na uandikishaji wa daftari la kudumu la wapiga kura kwa ajili ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.