Dar es Salaam. Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) nchini Tanzania, Rais John Magufuli amewataka viongozi wa mikoa wa chama hicho kutokuwa na majina yao mfukoni katika mchakato wa kura maoni kuwapata wagombea wa udiwani na ubunge.
Rais Magufuli ameyasema hayo leo Ijumaa Januari 24, 2020 jijini Dar es Salaam alipokutana na viongozi wa mikoa, wilaya na jumuiya za chama hicho kutoka mikoa yote nchini.
Amewataka viongozi hao kuweka mbele maslahi ya chama hicho kwa kuchagua wagombea wenye sifa na wanaokubalika kwa wananchi.
Amesema ndani ya CCM, kila mtu ana haki ya kuchagua na kuchaguliwa.
"Wakati wa mchakato wa uchaguzi, tusiende na majina mfukoni, kwamba huyu ni wa mwenyekiti, huyu ni wa katibu. Wakati mwingine unakuta mwenyekiti na katibu mkuu wanagombana. Tuweke maslahi ya chama chetu mbele," amesema Rais Magufuli.
Rais Magufuli amesema chama hicho kiko imara, viongozi wasibabaishwe na kelele ndogo za washindani wao ambao nguvu zao zimekwisha.
Habari zinazohusiana na hii
- Magufuli: Sitaki CCM iwategemee matajiri - VIDEO
- Magufuli ataka viongozi CCM kuitetea, kuisimamia Serikali
- VIDEO: Viongozi 1,780 wa CCM wahudhuria mkutano ulioitishwa na Magufuli