Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

VIDEO: Bashe afunguka kuikosoa Serikali ya Tanzania, amtaja Lowassa

Video Archive
Mon, 24 Jun 2019 Chanzo: mwananchi.co.tz

Dodoma. Mbunge wa Nzega Mjini (CCM), Hussein Bashe ametaja sababu tatu za kwa nini anaikosoa Serikali akitaka jambo hilo kutohusishwa na uamuzi wake wa kumuunga mkono Edward Lowassa katika mchakato wa chama hicho tawala kupata mgombea wake wa urais katika uchaguzi mkuu wa mwaka 2015.

Bashe alitoa kauli hiyo baada ya kuulizwa swali kuhusu namna anavyozungumza mambo mbalimbali kuhusu Serikali na kutafsiriwa kama mkosoaji.

Aliulizwa pia kama suala hilo lina uhusiano wowote na uamuzi wake wa kumuunga mkono waziri mkuu wa zamani, Edward Lowassa katika mchakato wa kumpata mgombea urais ndani ya CCM katika uchaguzi mkuu 2015.

Lowassa alijitosa katika kinyang’anyiro cha kuwania kupitishwa na CCM kuwania urais lakini yeye na wenzake 33 walikatwa katika mbio hizo baada ya Kamati ya Maadili ya CCM kuona hawana sifa ya kugombea. Julai 25, 2015 alijiunga na Chadema na kupitishwa kuwania urais na kushika nafasi ya pili nyuma ya Rais John Magufuli.

Machi Mosi, mwaka huu Lowassa alitangaza kurejea CCM baada ya kupita siku kadhaa tangu alipokutana na Rais John Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

Kwa mahojiano yote Usikose nakala ya Gazeti la Mwananchi Juni 23,2019, Pia tizama video hii-

Pia Soma

Chanzo: mwananchi.co.tz