Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uwanja wa MO Simba wazuiwa kutumika

MOS Uwanja wa MO Simba wazuiwa kutumika

Wed, 10 Jun 2020 Chanzo: www.tanzaniaweb.live

Shirikisho la soka nchini TFF, limezuia uwanja wa klabu ya Simba (Mo Simba Arena) uliopo Bunju Dar es salaam kutumika katika mechi za kirafiki za klabu hiyo kwa kuwa ni maalumu kwa mazoezi tu.

Taarifa ya TFF iliyotolewa leo Juni 9, 2020, imeeleza kuwa mechi za kirafiki kwa vilabu zimerejeshwa baada ya kuzuia hapo jana kutokana na vilabu kutofuata muongozo wa Wizara ya Afya na Habari kuhusu usalama kwa mashabiki.

Uamuzi huo umefikiwa baada ya kukutana na vilabu vya Simba, Azam FC, Yanga, Transit Camp na KMC na kuahidi kufuata muongozo huo katika mechi zinazofuata.

Chanzo: www.tanzaniaweb.live