Habari

Burudani

Michezo

Biashara

Afrika

Live Radio

Nchi

Kijamii

Lifestyle

SIL

Uteuzi mjumbe mwanamke ZEC waikuna Tamwa

Thu, 21 Jun 2018 Chanzo: mwananchi.co.tz

Zanzibar. Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake, (Tamwa), kimempongeza Rais wa Zanzibar, Ali Mohamed Shein kwa kuteua mwanamke mmoja kuwa mjumbe wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC).

 

Dk Shein alifanya uteuzi huo jana na kumteua Jaji Mkuu mstaafu wa Zanzibar,  Hamid Mahmoud Hamid kuwa mwenyekiti wa ZEC.

 

Pia aliwateua wajumbe wengine akiwamo Jokha Khamis Makame. Kuteuliwa kwa mwanamke huyo kumefanya Tume hiyo iliyopata wajumbe wapya karibu na uchaguzi wa mwaka 2020 kuwa na asilimia 14.2 ya uwakilishi wa wanawake.

 

“Tamwa Zanzibar inachukua nafasi hii kumpongeza pia mjumbe huyo (Jokha) aliyeteuliwa na kumtakia kila la heri, busara, uweledi na haki katika utendaji wake,” imesema taarifa hiyo ya Tamwa iliyotumwa kwa vyombo vya habari leo, Juni 21.

Taarifa hiyo iliyosainiwa na Mkurugenzi wa Tamwa Zanzibar, Dk Mzuri Issa imeongeza: “Ni vyema pia vyama vya siasa kuanza kujitafakari na kuangalia kuwa wanawake ni wadau wa maendeleo kama wanaume hivyo wanahitaji kushika nafasi muhimu za maamuzi ndani ya vyama vyao.”

 

Chanzo: mwananchi.co.tz